Mwanamke na vya Ubwete

twijuke

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
547
Reaction score
252
Hili ndo jicho langu kwa mwanamke. Wana JF akina mama, ni mama zetu,ni shangazi zetu, ni bibi zetu, ni dada zetu, binfsi nawapenda nakuwaheshim, Nawaona kwa jicho la kupenda sana nafuu, mfano amekaa mahali panapouzwa chakula akiwa mezani, huyu mwenzetu wakati wa malipo aatafurahi kuambiwa chakula ulichokula tayari kimelipiwa, pasipo kujali nani amelipa.
Mwenzetu huyu amemwita mwendesha bodaboda, pasipo kujali umbali wa safari wakati wa kufanya malipo mtu wa bodaboda anasema dada au mama we nenda tu, hapo ndo utasikia mwenzetu anafurahi na kusema jamani asante, na badaye anasimlia kwamba huwezi amani Yule kaka amenitoa sehem flani na kunileta hapa bule, ebu tafakari chombo hiki kinatumia mafuta mwendeshaji anafanya kazi hii kwa ujira hata kama ni mmiliki wa chombo hiki lakini anafanya kazi hii kwa ujira.
Mwenzetu huyu yupo kwa mchoma chipsi anafurahi kama si kupewa bule basi ajaziwe sahani tofauti na kipimo wanachopimiwa wengine. Akienda gengeni atajaziwa nyanya nahapa ndo utasikia anamsifia Yule kaka muuza genge, yaani huwezi amini manyanya yote haya nimelipa sh. 500 tu, anaona fahari kupewa bule au kujaziwa, wengine akikuta dukani mtu ambaye hakumzoea anaondoka kwa kukwepa kupimiwa kipimo halisi na hapa ndo anasema amepunjwa, anasahahu kuwa mnunuzi naye kapimiwa kipimo halisi.
Mwenzetu huyu amekuita umfanyie kazi, pasipo kujali umetoka umbali gani anatamani ukimaliza kazi umwambie usijali kwakuwa kazi ni ndogo, hapa sasa ndo utasikia jamani asante siku nyingine nta kuita tena. Naamini hata sehemu kubwa ya mahusiano ya kimapenzi imetokana na mlango wa nafuu, mwanamke anaweza kuwa hampendi mtu lakini hii pokeapokea au bebwabebwa chaweza kuwa chanzo cha kujenga mahusiano. Hii ni sehemu ndogo ya mambo mengi yanayohusu KE.
Huu ni mtanzamo wangu, pia naomba niweke wazi kuwa si wote bali sehemu kubwa wako hivi.
Nadhani wataalam wa masuala ya tabia watanisaidia, au kuwasaidia watu wa mtazamo kama wangu hii inatokana na nini. Na omba nisamehewe kwa yeyote nitakaye kuwa nimemkwaza.
 
mie mtaalamu wa tabia lakini siwezi kukusaidia chochote na huyo mwanamke hajaomba kufanyiwa yote hayo bali ni hao wanaojitolea ss tatizo liko wapi?
 
mie mtaalamu wa tabia lakini siwezi kukusaidia chochote na huyo mwanamke hajaomba kufanyiwa yote hayo bali ni hao wanaojitolea ss tatizo liko wapi?

sorry mtaalamu wa tabia ?
au sijakuelewa?
wanakuwaje wataalamu wa tabia?
 
Ndo walivyoumbwa na mindset izo.Those creatures are typically receivers by nature.
 
Halooooo! Raha ya kuhongwa si kile uongwacho bali ukweli kuwa Umekubalika na mhongaji!
 
Uuuhh aiseee kunahitajika jukwaa la mipasho maanake...ngoja nijiondokee mie
 
Uuuhh aiseee kunahitajika jukwaa la mipasho maanake...ngoja nijiondokee mie

Dawa ya mipasho kama hii ni kuipotezea ikose wachangiaji..... niko nyuma yako kwa mwendo wa kasi!!!
 
Xaxa ww unaumia nn au huo ubwete unautaka ww, funguka ueleweke kjana coz hao kina mama hawajaomba n viherehere vyao wnyw, we jamaa unapoelekea umbea utakuua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…