Mwanamke bora humsapoti mumewe

Makau Js

Member
Joined
May 25, 2017
Posts
93
Reaction score
233
Mwanamke mzuri na mwenye hekima na busara siku zote hubeba baraka na mafanikio ya mume wake, Siku zote mwanamke bora humsapoti mumewe kwa hali zote shida na raha.

Tatizo huja wanawake wema na wazuri hupata wanaume wasiowajali na kutowathamini wake zao, uzuri wa mwanamke hupotea kwa simanzi apatayo kwa mume wake.

Mwanamke mwenye hekima na busara aliyemuaminifu kwa mume wake akiwa analalamika kwa haki yake ya msingi hufunga baraka za mwanaume asiyemuaminifu na na asiyemjali wala kumthamini mkewe.

Matatizo mengi kwenye familia yanatokana na mume au mke, ndoa yenye furaha na amani huwa ni zenye baraka na mafanikio ya kila siku.

Mwanamke unatakiwa kumuomba Mungu akupe hakima na busara ili kuweza kuwa mjenzi mzuri wa familia sababu asilimia kubwa ya wanaume ni wabinafsi na wasiokubali kukiri makosa yao mapema.
 
Wanawake hao unawazungumzia katika thread kwa Tanzania wapo 10%..!utamjuaje?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…