Watu wangu wa Mwanza mambo vipi? Ilemela, Buzuruga, Mabatini, Buhangwa, Airport..!!!!
Baada ya kuingia tu jijini kitu cha kwanza nimeomba nipelekwe kwenye uli mti uliowahi kujadiliwa humu JF, mti kunyonga. Yale maneno yameniuma sana karibia nirudi zangu nilikotoka kwa hasira.
Mimaneno imekaa kivitisho vitisho dhidi ya wanaharakati, wapingao kukandamizwa na serikali dhalimu.
Picha nimeichukua usiku so kama maandishi hayaonekani vizuri tuwiane radhi.
Miaka mingapi huko mbele wataweka minara kwenye makaburi ya watu waliouwawa kwenye maandamano ya Arusha, Zanzibar na kwingine kutakakoibuka na kusema, "Hapa ndipo walipozikwa wahaini dhidi ya Serikali".