Mwanafunzi afariki baada ya kupigwa na Mwalimu

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,813
Reaction score
63,268

Mwanafunzi afariki baada ya kuchapwa na mwalimu Kenya
Wazazi katika kaunti ya Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya mwalimu kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi akafariki.Mtoto huyo inaarifiwa alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai. Alifariki alipokuwa anapelekwa hospitalini.


Wazazi hao waliandamana kwa amani wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
Hata hivyo polisi waliweza kumkamata mwalimu huyo na kumpeleka kituoni huku uchunguzi ukianza kufanywa.
Mtoto huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi ya Roka Preparatory.
Inaarifiwa alizirai baada ya mwalimu kumchapa kwenye kisogo.


Wazazi hao waliokuwa wanalalamikia kile wanachosema ni wanafunzi kuadhibiwa vikali kwa makosa madogomadogo walitaka mwalimu huyo achukuliwa hatua kali kwa kitendo hicho cha kumchapa mwanafunzi ambacho kimeharamishwa katika shule zote nchini Kenya.
Wengi wa wazazi wenye watoto wao katika shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule nyingine.
Kenya iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi iliyopita. Ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na kuwajeruhi kukithiri.


chanzo;BBC
 
R.I.P. Dogo ila alimchapa hadi kufa au alimsababishia kifo?
 
Mtoto akikosea aadhibiwe sawa lakini kuna maeneo ya kuchapa mtoto,kwenye kiganja au kwenye makalio.
Kuna walimu wanachapa hovyo kama anamkomoa mtoto,sasa huyu amempiga kichwani kweli!! Hata kama kifo kina sababu lakini fimbo za hovyo kwa mtoto si nzuri.
Pole kwa wazazi wa huyo mwanafunzi.
 
huyu mwalimu lazima achukuliwe hatua za kisheria! utampigaje mwanafunzi kichwani?
 
Kumchapa mtoto ni kumuelimisha ila tuangalie hizo adhabu tunazo wapa watoto je wanastahili nazo
 
hii nayo mpya hakuwa mgonjwa kweli huyo
 
Mbona Plasmodium wa Malaria ikiua hawaandamani!!

Kwani walijua kifo chake kingetokana na nini?

Mwalimu amemalizia tu sema huyo alikuwa na kifo mwilini.
 
Jamani hakukusudia mara nyingine wanafunzi wanapoadhibiwa wanasumbua kwa woga hivyo fimbo huweza kumpata sehemu mbaya
 
Mwalimu ameshapewa kesi ya mauaji
 
:A S 465:Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.....Hiyo yote ni misongo ya mawazo......mishahara midogo,hasira toka nyumbani kwa mkeo au mmeo wana malizia kwa wanafunzi. kodi za nyumba kubwa..MUHIMU WALIMU TUWE MAKINI NA MAAMUZI SAHIHI WAKATI WA KUTOA ADHABU KWA WANAFUNZI...:A S 465:
 
Jamani hakukusudia mara nyingine wanafunzi wanapoadhibiwa wanasumbua kwa woga hivyo fimbo huweza kumpata sehemu mbaya

Acha utani wakati wa maskhara bana ulenge ---- upige kichwa ati! !!?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…