Mwagane yeya !! Mwagane yeya !! Daaah


jukwaa la sports ni jukwaa la watu waungwana,huku tunaburudika hatuleti dhihaka,chuki na ujivuni.
 
Gentamycine umekuwa na mengi kama jina la dawa uliloandika ,, mi nimejaribu tu kusema na kuweka wazi kile alichofanya mwagane yeya na kumpa tu ushauri , na pia kumpongeza , hakatazwi kwenda yanga wala simba kwa maslai yake .
atakuumiza kichwa huyo bradha.
 
Sasa hivi hizi timu mbwa simba na yanga zinatafuta kila njia kuihujumu na kuipoteza mbeya city.hazijui mpira zaidi ya fitna na ungese tu.
 
Gentamycine kubali kushindwa huna point mkuu!
Kwa kusema kuwa ligi ina wenyewe ni sawa na kusema timu zingine zisihangaike na mpira kwakuwa historia inaonyesha kuwa hazitafika mbali.Hayo siyo tu mawazo ya kipuuzi bali pia ni mawazo ya kizamani yenye yaliyojaa uwoga na kukatisha tamaa!successes always come through struggle mzee! Wacha watu wajifue, wapambane na kisha wasonge mbele kimpira! Kasumba ya usimba na uyanga ndo zinadidimiza mpira wa nchi hii! Nashangaa hutaki changamoto kwenye maendeleo we vipi? Mtu wa wapi wewe????
 

Mkuu nipo nawewe manake hao mbeya city kelele tu wenye mpira wao bado hawajaanza kazi yao simba na yanga
 
Duuu, umesema Mbeya city wakafanishwe na MAKALIO?, naona una hasira sana na Mbeya city, sasa bro hizo zilikuwa ni sare tu, mzunguko unaofuata mkikutana na CITY lazima mkalie mti, ...manina.
 
haya yote ni sababu ya hat trick ya mwagane yeya..
 
mkuu mambo ya umri wa wachezaji wetu usiwe unauliza utaishia kudanganywa tu ukute ataitwa U17 TEAM

Lol, kuuliza muhimu kaka. Akiitwa U-17 tunaguna, maana kuna mtu kashasema jamaa ni mwalimu, kwahiyo hapo tunahesabu si chini ya 23. Ninauliza sababu ninashangaa mchezaji kama huyo anakuwa wapi muda wote asionekane? Unajua magoli ya vichwa aliyofunga amepima vizuri sana, na hajahangaika kuruka. Striker mwenye mwili kama yule ni lulu sana, ingawa sijaona akicheza vipi, lakini alivyofunga inaonyesha ni striker anajua anachofanya (labda umri uwe umekwenda tu). Nikiona striker ana mwili mzuri halafu halafu amechelewa kutoka na hatumii potential yake vizuri, inasikitisha....mfano John Bocco.
 
Mkuu katika vitu vilivyofanya nisikitike ni taaluma yake, ukiangalia ye aliyakiwa awe mchezaji siku nyingi, mfumo wetu hautoi nafasi ya kuendeleza na kukuza vipaji, pata picha kama toka udogo wake angelelewa na kukuzwa kisoka kwenye academy maalum angekuwa wapi?, kama ni mwalimu manaake kweli atakuwa na 23yrs na zaidi, ina maana muda wote kipaji chake kilikuwa hakionekani kwa sababu ya mfumo mbovu, mtaani kuna wachezaji wengi sana ila ndo hivyo siku hizi hata vile viwanja vya vumbi wanageuza masoko
 
viva Mbeya city
kutoka ligi daraja la kwanza mpaka ubingwa ligi kuu

ha ha ha ha haaaaaa....unanifulaisha sana "kutoka ligi daraja la kwanza mpaka bingwa ligi kuu" das ram yanga afrika wanakuangalia tu unachukua ubingwa,inamaana hawa jamaa watakuwa wamefilisika kiasi gani mpaka wakakosa hela yakununu mechi hili wasiwe mabingwa wao.
 
Tena hat trick na timu ngumu kama azam....

kwangu mimi ni mchezaji wa kawaida sana sana sana tu,hila mungu haalimpa bahati nzuri alichokuwa anfanya kwa siku hile alikuwa anpatia...."utajiuliza kwanini awe mchezaji wa kawaida,apate bahati cku hy na alichokuwa anafanya siku hy awe anapatia" kwani kama sikosei anacheza mechi ya13 ana magori manne kwa maana kabla ya hiyo alikuwa na gori 1....so mechi hz nyingine alikuwa wapi..? leo hii hawe forward mzuri kwa mechi mmoja tu..!?ndio maana nabaki pale pale mungu alimjalia na hakampa na bahati kwani kila alichofanya akawa anapatia naishia hapo kwake MWEGANE YAYE a.k.a mwalim......nimependa magori yake pia niimependa MBEYA CITY...i am nomber one fans of AZAM FC.
 
Huyu jamaa kafunga magoli mazuri sana , umeonyesha namna ambavyo mfungaji anapaswa kuwa , usiishie hapo ongeza bidii mpira wa tz haulipi kiivyo ongeza bidii angalia mbele!

sio mbele tu hata hakiangali nyuma haendi kokote na magori yake manne mechi 13.
 
Mkuu nipo nawewe manake hao mbeya city kelele tu wenye mpira wao bado hawajaanza kazi yao simba na yanga

wenye mpira wao.!!!????

au wenye uchawi na fitina zao.!!
 
Mkuu nipo nawewe manake hao mbeya city kelele tu wenye mpira wao bado hawajaanza kazi yao simba na yanga
Wataanza lini? Hao jamaa (Simba na Yanga) mwaka huu mmoja wao (kama sio wote) anaweza akachambia tindikali. Azam até no morte.
 

Jamaa ana akili sana ya mpira magoli yake ya vichwa naweza kuyafananisha na yale aliyokuwa akifunga luis garcia (czech, liverpool), au kama lile alilofunga dzeko (wolfsburg vs manchester united. Zaidi ya magoli ya kichwa hata lile alilofunga kwa mguu alitumia umakini mkubwa, baada ya kusukumana na Morad kipa alijua jamaa atasubiri mpira udunde lakini jamaa akaupiga kabla ya kudunda kwa ustadi mkubwa sana. Hata kama baadhi wanaona ilikuwa ni fluke ya mechi moja bado ni complete striker.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…