Mvutano wa kiakili

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,545
Reaction score
59,365
Kwako Binti na Mwana wa Afrika.

Elimu za Dunia zinafundisha watu, kuenenda kwa akili/kutumia akili zaidi.

Elimu za kiroho zinahimiza Unyenyekevu/kuenenda kiroho/kutumia uwezo wa ndani wa kiakili.

Kawaida ukitumia sana akili ya ubongo kuna matokeo tofauti na ukitumia akili ya kiroho/ uwezo wa ndani zaidi wa kiakili, nako kuna matokeo tofauti.

Ukiwa ni Mtumiaji zaidi wa akili ukijaribu kutumia moyo, akili huwa inagoma kukubaliana na akili ya rohoni.

Hali hizi ndizo huleta matabaka ya kufanya, kuwe na watu wa hali tofauti. Kuna Matajiri na Masikini, Kuna wajinga na werevu, kuna wasomi na wasioelimika, wabishi na waungwana.

Ukiona kila jambo unashindwa na Dunia, ujue uwezo wako wa kumudu Dunia, hauendani na matumizi ya akili ya kawaida bali uwezo wako upo katika akili ya kiroho. Hivyo inatakiwa ibadilishe mfumo.

Ukitumia akili tofauti na ulivyo zoea, itakubadilishia namna unavyoyaelewa maisha na hivyo kuona fursa zinazoendana na wewe na za kukufanikisha.

Ukiona unashindana na roho, ujue uwezo wako upo katika akili ya kawaida na wewe unatumia akili ya kiroho ambayo haiendani na mtizamo wako kuhusu maisha na mambo ya kidunia.

Masikini wengi wa Dunia hii, ni wanyenyekevu wa kiroho. Wakati matajiri wa Dunia hii, ni wanyenyekevu wa kiakili.

Kama ulisha wahi kujiuliza, kwanini walokole na wenye kufuata sana dini ni masikini, nadhani umeanza walau kupata majibu.

Sina maana ukienenda sana kiroho, unakuwa masikini Lah!. Wapo wanyenyekevu wa Kiroho ambao ni matajiri sana.

Ni nadra kwa walioshika nafasi kubwa darasani, kwa kuwa na uwezo mkubwa kiakili, kuwakuta wakiwa hivyo Katika uwanja wa Kiimani, kanisani, misikitini n.k.
Ila utawakuta katika uwanja wa Elimu za dunia, siasa, sayansi, na ndiyo viongozi katika mifumo ya kidunia.
Wanaokuwa wakishika nafasi ndogo darasani, wao huongoza katika maisha ya kawaida. Ndiyo sababu ya matajiri wengi kuwa sio wasomi.

Mvutano wa kiakili ni pale Dini zinakulisha ili kukujenga rohoni, na Elimu ya Dunia inakulisha ili kukujenga ubongoni.

Hakuna mwenye uwezo wa kujilisha vyote na kufanikiwa vyote.

Ndiyo maana, wajuzi wa elimu za kidunia, na pia ni wajuzi wa elimu za kiroho hukosa vyote. Sababu Elimu ya Kiroho ni kinyume cha mfumo wa Elimu za Kidunia.

Watu wanaofanikiwa kwa vyote, ni watu ambao wanatumia akili za kiroho, sababu, akili ya nje ni kopi ya akili ya Rohoni.

Akili ya kiroho haidanganyi, ndiyo yenye kubeba uhalisia wako, unaoendana na namna ya kuyakabili maisha na mambo ya kiroho.
Akili ya kiroho ndiyo imebeba nguvu za kipawa chako, na mustakabali wa hatima yako.
Hivyo ukiona unasumbukia maisha na kufanikiwi, ni wazi umeiacha njia ya asili yako na unavutwa na njia ya mfumo wa dunia ambao ni asili ya wanaofanikiwa katika eneo hilo.

Mafanikio ni kutawala rasilimali za Dunia.

Kipawa/zawadi ndicho kitakufa Na Kipawa ndiyo zawadi pekee uliyopewa na Muumba ili uweze kuongea na Ulimwengu.

Kila mmoja amepewa kipawa chake, na ni tofauti na mwingine.

Kasheshe huja jinsi ya kuielewa na kuifuata asili yako, kwa kutumia asili yako ya kiroho.

Leo nilitaka kukujuza juu ya uwezo wako wa ndani na uwezo wako wa nje.

Akili yako ya ndani na akili yako ya nje.

mfululizo unaofuata nitakujuza jinsi ya kuufikia, kuutumia kiroho na kimwili ili kukufaidisha kiroho na Kimwili.

Tuwe pamoja,
 
Waiting
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…