MUZIKI NA MALEZI
Mzazi lazima umwambie mtoto wako kuna nyimbo hatakiwi kuzisikiliza wala kuziimba.
Kwenye eneo la muziki na malezi wazazi mmejisahau sana.Wengi mmeweka mkazo katika kuzuia watoto kutokuangalia picha za ngono lakini je umeshawahi kuwaambia nyimbo kama hizi sitaki uzisikilize, kuziiimbaau au kuangalia video zake?. Sasa hivi kwenye muziki kuna uharibifu mkubwa unafanyika katika kuharibu maadili na tabia za watoto na hata watu wazima.
Kwanza Ieleweke muziki ni fani kama fani nyingine sio uhuni lakini kama watunzi waimbaji upeo wao wa kufikiri ni mdogo basi waimbaji hawa sasa hivi hawaimbi tena nyimbo za mapenzi, bali wanaimba ngono nadhani utanielewa kuna utofauti wa (love na sex)
Muziki ukiwa moja ya kazi ya fahisi kazi yake ni kuonya, kuelimisha, kuburudisha,kuelekeza njia sahihi.
Ndio unakuta wazee wetu kwenye bendi waliimba nyimbo hizo, waliimbazenye maudhui tofauti kuhusu Amani, ukombozi, kuonya kujihusisha na mapenzi shuleni,waliimba mapenzi na hawakuimba ngono,waliimba nyimbo ambazo hata kwenye mitihani wanafunzi waliulizwa maswali kujadili fani na maudhui.
Je wasanii wa leo ndio wanachokifanya? Au ndio kwenda na wakati au uvivu wa kufikiri hata kama muziki ni biashara kwa hiyo kuimba sex ndio biashara?unawaacha watoto wangalie TV muziki wowote kwenye simu wana sikiliza muziki wowote tu, Je umeshawahi kumuonya au kumuelimisha madhara ya hiyo miziki au unasubiri madhara yatokee ndio ukumbuke shuka wakati kumekucha? Ndugu zetu wa habari nyinyi hizi mambo ndio mnao zisambaza kupitia redio na TV zenu hivi ndio maadili ya kazi yenu, au hadi BASATA waufungie wimbo? Je nyie mnatoa sapoti gani kwa BASATA na jamii?msimamo wenu uko vipi kuhusu hili suala?
Kwanini watoto hawatakiwi kusikiliza baadhi ya nyimbo zisizo elimisha
1.hazikuzi ulewa wao wa kufikiri
2.zinaharibu ufahamu wao wanaanza kuwanza ngono muda mwingi
3.wanajenga udadisi wa wanayoyasikia kwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo
4.Muziki nguvu na ushawishi kama mtoto anasikiliza nyimbo hizo zitamuathiri kitabia
-kuna mabinti wamepoteza usichana wao kwa kusikiliza nyimbo za ngono zikawashawishi na kujikuta wamepoteza usichana wao
-Ona nguvu ya muziki mwanamuziki wa Zaire Franco alipofungwa na Rais Mobutu alikuja kutunga wimbo uliomsifia kiongozi huyo na huo wimbo ulikuwa sababu ya kumtoa jela hadi kukaribishwa ikulu Raisi aliupenda sana huo wimbo unaitwa (Candidat na biso Mobutu)
- kwenye vitabu vya dini huko ndio kabisa mifano ipo mingi unakupumbuka habari ya Paulo Sila pia walipokuwa Jela walipomsifu Mungu nini kilitokea.
5.Hizi nyimbo za ngono zinawachochea vijana wetu kushiriki ngono mapema
6.Muziki una nguvu hata ya kumfanya mtu atoroke nyumbani, shuleni hata kula ada ya shule ilimradi akaiburudishe nafsi yake kwenye muziki.
Kwa hiyo Muziki unaweza kutumiwa vizuri au vibaya lakini ni jukumu la wazazi,walezi na walimu kuwaelimisha watoto lazima wajue nyimbo zinazowafaa na zisizo wafaa na uwape na sababu. Inasikitisha kama hata kwenye vipindi vya Tv na redio mtoto akiulizwa kama anaweza kuimba basi nyimbo atakazoimba ni hizohizo huku ni kuwaaribu watoto lazima ukweli tuuweke wazi. Unaweza share ili kusaidia malezi ya watoto kupitia muziki
By Jeremiah
Musician
Music Educator
Music analyst
Song writer
Insta.Jerry_viola
Sent using
Jamii Forums mobile app