mi mwenyewe huwa napenda documentaries na hivi karibuni nilikuwa na donwload documentaries zinazohusu mazingira mojawapo inaitwa. gasland. hii inahusu uchimbaji wa gesi asilia huko marekaini na athari zake kwa mazingira. makemikali ya kuchimbia gesi yaliingiliana na maji ya ardhini na kusababisha kansa na pia gesi ilichanganyikana na maji hadi maji ya bomba ukiyawasha na kiberiti yanawaka. nilichojifunza ni kwamba m arekani wana gesi asili nyingi sana, pia wanawalipa watu wenye ardhi yenye gesi pesa nyingi sana kuliko huku ambapo watu huporwa ardhi, pia nikajiuliza kama wanaweza kuhatarisha afya za watu wao je vipi zetu sisi?. nikaogopa sana kuhusu miradi yetu ya uranium .