Must read: Tubadilike

Mdharuba

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2011
Posts
824
Reaction score
522
Napenda kutoa pole kwa familia zote zilizokutwa na majanga haya ya misiba kutokana na ajali mfululizo zinazoendelea kutokea hapa nchini kwetu. Wengine wamepoteza watu ambao ni viungo muhimu katika familia, na wengine wamepata vilema vya maisha ikiwa ni pamoja na kukatika miguu au mikono na viungo vingine.
Kwa masikitiko makubwa natoa pole nyingi sana kwa hawa Watanzania wenzangu. Mungu azilinde familia hizi zilizokumbwa na majanga na awape utulivu, uvumilivu pamoja ujasiri katika kipindi hiki kigumu. Nadhani Mungu ana makusudio yake makubwa katika matukio haya yanayoendelea kuiandama nchi yetu. Naamini Mungu bado anatupenda na anatutakia mema tu sisi viumbe wake dhaifu kabisa ambao hatuwezi kuzuia hata moja katika yale ambayo ametupangia yatukute.
Ila kuna jambo moja bado linanitatiza saana mimi katika jamii yangu...Watu wanapoanza kuhusisha matukio haya ya ajali na imani za kishirikina, freemasons na uzembe wa madereva. Mimi nina msimamo tofauti kidogo, na leo naomba kujadili na nyinyi.
Tuanzie hapa kwa madereva,..
Nimeshuhudia ajali kadhaa zilizotokea na baadhi ya madereva kupoteza maisha,
Sasa mimi naanza kujiuliza, dereva huyu analaumiwa kwa kipi?? Uzembe wake ni nini?? Yeye ni binadamu mwenye akili timamu, na yupo humo kwenye gari akiwa amezibeba roho za watu zaid ya 65 na ya kwake ikiwemo, limetokea tukio la ghafla linalofanya gari ipoteze muelekeo, anajaribu kunusuru maisha ya watanzania wenzie mpaka na yeye anapoteza roho yake, sisi bado tunalaumu dereva mzembe, kwa lipi haswa??!!
Huenda dereva alikua akienda mwendo kasi sana kabla ya ajali, lakini sisi abiria ambao tupo 65 ndani ya basi tulishindwa kung'amua hili mapema ili tumripoti dereva kwa vyombo husika kama atakataa kupunguza mwendo, mpaka ajali imetokea ndo tunasema eti dereva alikua kasi sana,, How comes??!!.
Nimemsikia dereva mmoja leo asubuhi kwenye redio akisema kuwa huwa wanapata karipio kali wanapoendesha spidi inayokubalika kisheria kutoka kwa wamiliki wao. Unafikiri hawa wamiliki wa mabasi hawajui kuwa kuna ajali?? Wamiliki hawa ambao mabasi yao yakikamatwa wanapiga simu na kusema "Mwache huyo aende" na gari ikaruhusiwa kuendlea na safari unafikri ni wamiliki wa kawaida??!! Sisi tumezoea kuwaona na kuwajua WASIMAMIZI tu wa mabasi na sio WAMILIKI. Yule Prof aliyeingia kwenye skendo ya ESCROW alipoulizwa zile pesa umezipeleka wapi? Alisema niliingiza katika mradi wangu wa malori, wewe unamjua anamiliki lori zipi??!! Hebu tuachane na hiki kipengele, ni kirefu.
Turudi hapa katika uchawi na freemason.
Najiuliza swali moja muhimu, na ningependa hata wewe unayesoma ujiulize, Hivi Mungu unayemuamini wewe ni mdhaifu kiasi hicho hadi viumbe wake wanatolewa tu roho kizembe na freemason na yeye yupo tu?? Yaani hawa freemason na wachawi ndo wana uwezo huo wa kutoa roho za watu kiasi hicho na huyu Mungu tunayemuamini na kumsifu kila siku anaangalia tu??!! Labda nkuulize swali jingine, Kuna jambo lolote ambalo linaweza kutokea pasipo ridhaa ya huyu Mungu wako unayemuamini??!! Uwezo wake ni mdogo kiasi hicho?? Na kama kila kitu anakiratibu yeye kwanini tusirudi kwake na kumuomba atupunguzie hizi adhabu za vifo vya ajali badala ya kuwapa madaraka wasiyostahili hawa tuwaitao freemasons na wachawi??!!.
Mwisho, namalizia na watumiaji wenzangu wa 'Social Networks'...
Hebu jamani tujifunze kuwa wastaarabu,
Kuna vitu vinanikera sana mimi, watu wamekua mashabiki wa vifo vya wenzao, kila linapotokea tukio watu mbio mbio kupiga picha na kuzirusha mitandaoni pasipo hata kutoa msaada kwanza.
Tumekua watumwa wa simu zetu siku hizi, sielewi ni kwanini..!! Ajali moja basi utatumiwa picha mpaka uone kichefuchefu😪
Wengine wakishiriki kusambaza taarifa za uongo ambazo hata hazijathibitishwa, kila mtu amekua 'reporter' na hujui haswa msemaji mkuu wa matukio haya ya ajali ni nani kwa sasa hapa Tanzania. Sasa hivi utaambiwa ajali imetokea sehemu fulani watu 40 wamekufa, baadae nikiangalia taarifa ya habari kwenye tv ajali hiyo haijaua, ----!! 😚
Hivi mnajisikia raha gani kuripoti ripoti tu matukio bila hata ya uthibitisho??!! Kuwa na simu yenye Whatsapp ndo imekua shida??!!
Wengine wanatuma picha za ajali za miaka minne iliyopita, hawajielewi maskini!!
Kuna wanaonikera zaidi ambao wao kupitia majanga haya ndo wanapopata ujiko kwa kutunga vistori vyao vya kipuuzi vikikuweka 'attention' na kudhani kuna ajali kumbe mwisho ni upuuzi mtupu!!. Hebu tubadilike watanzania wenzangu, ajali zilikuwepo tangu kipindi hicho ambacho simu za Camera hazijafika Tanzania,, kukithiri kwa ajali siku za karibuni ni suala la kumuomba Mungu atulinde na majanga haya baada ya sisi wenyewe kuchukua tahadhari juu ya mambo ambayo huenda kwa namna moja ama nyingine yanapelekea ajali hizi kutokea.

Naomba kuwasilisha!!

J.K Mdharuba (Mr).
 
Duuh!
nimeshindwa kumaliza kusoma..
 
Jikaze kaka,, kuna mengi humo
 
Kuhusu mungu kuacha freemason na wachawi kusababisha ajari na mungu kutosaidia,ipo hivi,mungu amemuachia shetani nguvu ya kutupepeta km ngano,na mungu alishatoa miongozo ya kujilinda ukiifuata mungu atakulinda na kukuepusha na shetani hawezi lolote ukifuata matakwa ya mungu,usipo fuata mungu huacha yote yatokeebjuu yako,ndo maana ni muhimu sana kila siku kila saa kujiweka chini ya ulinzi wa mungu,
 

Unaamini shetani kwa uwezo aliopewa anaweza fanya vitu ambavyo Mungu hajaviratibu??
 
Hakuna cha kumsingizia mungu wala shetani Ni sisi wenyewe ndio tunafanya ajali kutokea
 
Hakuna cha kumsingizia mungu wala shetani Ni sisi wenyewe ndio tunafanya ajali kutokea

Kivipi?? Fafanua uwezo wa binadamu kusababisha ajali ukimueka mbali mungu kuwa hahusiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…