PostGE2025 Muliro: Tutaendelea kuwakamata wanaopanga njama za uhalifu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi katika kuimarisha ulinzi kwenye maeneo mbalimbali ya jiji.

Kwa mujibu wa taarifa ya siku ya Jumamosi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, SACP Jumanne Muliro hali ya usalama inaendelea kuwa ya kuridhisha, huku taarifa za raia zikisaidia kwa kiasi kikubwa kugundua na kuzuia mipango ya vitendo vya kihalifu.

Your browser is not able to display this video.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa maandalizi ya kiusalama yameongezwa kuelekea mchezo wa kimataifa wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaofanyika Jumapili, Novemba 23, 2025, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Petro Atletico ya Angola.

Jeshi la Polisi limewakumbusha mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kufuata taratibu, kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani, na kuhakikisha mchezo unafanyika katika mazingira salama na yenye nidhamu.
 
Kwa Sasa amekuwa na adabu baada ya kuona GenZ hawaogopi vitisho.Mwanzo alikuwa anaongea Kwa majigambo sana
 
Mahojiano ya Dw, aliyakambia maswalii, nakukata Simu.
 
Faki the mazafaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…