Lyagwa
JF-Expert Member
- Feb 3, 2013
- 1,639
- 900
Habari za siku ya leo. Natumai mtakuwa salama huku mkiendelea vema kulitumikia Taifa. Binafsi namshukuru Mungu kwa vile niko salama na ninaendelea na majukumu yangu ya kila siku.
Lengo la thread hii yenye lengo la kujifunza na kupata uelewa ni kuwa mimi binafsi nina mtoto wa mwaka mmoja na nusu sasa (1.5 years) ambaye tangu amezaliwa amekuwa akilia sana na kuonesha kuwa na maamivu makali sana katika interval mbalimbali, yaani anaweza akapatwa na hiyo hali let say leo, then ikatulia hata zaidi ya wiki mbili ingawa sometimes iliweza kutokea mfurulilizo say two days.
Wapo waliotuambia atakuwa anasumbuliwa na mshipa wa ngiri (hernia) nk, na hata tulipompeleka kwenye vituo vya afya walihisi hivyo. Amekuwa akipatiwa matibabu ya hapa na pale maana pamoja na hilo huwa anasumbuliwa na kifua assumption ikiwa hueanda ana pumu (asthma).
Lakini baada ya kuona trend haishuki, tuliomba kupewa transfer ili tuweze kuwaona Madaktari na vipimo zaidi. Baada ya maelezo kwa Dr. ndipo alipo suggest kipimo cha ultra sound na majibu yakaonesha mtoto ni kende moja ndio imeshuka chini kwenye zile kokwa zake na nyingine haipo, hivyo hiyo ndio inayomsumbua. Nilizoea kuyaona hayo wakati niko kijijini enzi za utoto unakuta ng'ombe ana pumbu moja ukiuliza unaambiwa lingine liko tumboni, sasa naiona tena kwa binadamu, tena mwanangu. Daktari ameshauri na kupanga tarehe ya operation, naendelea kumuomba Mungu atusaidie hiyo siku ifike na operation ifanyike salama.
Lengo mahususi la hii thread ni kutaka kujua sababu ya hiyo hali kutokea, madhara baada ya operation hata kama ikifanyika successfully kwa mtoto. Wataalamu naomba mnisaidie katika hili na pia itanisaidia katika kujenga confidence wakati nikisubiri tarehe ya hiyo kufika. Aidha pia inaweza kuwa darasa kwa watu wengine ambao labda walishakutwa na hali kama hiyo ama ambao wanaweza kukutwa na hiyo hali, maana wanasema hujafa hujaumbika.
Ahsanteni nategemea kusikia na kujifunza toka kwa wataalamu (Madaktari) na wenye uzoefu.