Katika harakati za kutafuta mtu wa kuanza naye maisha naona ugumu sana nimchague nani kwan nina marafiki wa kila aina.
moja, ninaye rafiki msomi sana a lawyer lakini simwelewi mwelewi kwan ni mkimya sana na nilishapewa scenario watu wakimya ni hatari sana.
mbili, ninaye mwingine ni msomi pia bachelor ya ualimu ni muongeaji sana na ana maneno mengi pia hajaariwa. Watu wenye maneno mengi pia ni hatari husambaritisha ndugu na ukoo mzima, pia akiajiriwa anaweza kupelekwa mbali na mimi mkata nyasi watanigongea wengine.
tatu, ninaye ambaye kaishia kidato cha sita ni mstaarabu ananiheshima pia ni mpambanaji wa mtaani ila shida familia yao ina maskini sana kiasi kwamba mkitafuta unaweza kuta kila siku unaliliwa shida zote zinazotokea pale kwa sababu ni watu fulani kama wanapatwa na mikosi sana.
Nne, ninaye wa aliyemaliza kidato cha nne yaan hawazi kama kuna future amekaa tu hana challenge yoyote ya maisha yaani kila kitu lazima uwaze na umtatulie kufuatana na mawazo yako.
Nimetafakari sana naona huu mtihani ni mgumu sana kuufaulu. Wengine wanashauri tafuta mtu mwenye kazi, wengine mara mweupe, wengine mara mweusi, mara mrefu, mara mfupi. Kwa kweli huu mtihani ni mgumu.
nimeangalia tena walioa mda si mfupi ndoa zimevunjika hata mwaka hamna.
mtihani huu ni mgumu kuufaulu..
karibu kwa maoni yako.