Mtazamo wa umaskini na utajiri katika jamii

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
427
Reaction score
577
Mtazamo wa umaskini na utajiri katika jamii

Umaskini sio laana ni daraja la kujifunza na kubadilisha , ukishakuwa na mtazamo huu utajilaumu kuzaliwa au kuwalaumu wazazi wako bali utatumia kama sehemu ya kujifunza na kubadilisha hali ya uchumi yako na wazazi wako au vizazi vyako.

utabadilishaje umaskini badilisha kwanza mtazamo wako, chukulia kama Mungu karuhusu kuzaliwa kwenye familia maskini ili wewe uwe ni wa kwanza kuondoa umaskini either katika familia yako au ukoo, ukiwa na mtazamo huu utafanya akili yako ianze kutafuta au kuona fursa na ukweli ni kwamba ukishakuwa na mtazamo huu fursa huo zinajitokeza.


Watu wengi katika jamii wana amini utajiri unatokana na uovu na wengine wana ridhika na hali zao za umaskini.

Ni muhimu utambua kuwa tajiri sio dhambi , Mungu kawapa utajiri watu wengi , anachotaka Mungu utumie utajiri wako kuwasaidia wengine, Mungu akikupa utajiri anaakikisha unaweza kuwa daraja kwa wengine kupata maitaji au msaada.

Mfano, ibrahimu, Mungu alimpa dhahabu na Mifugo, fedha nyingi na kuwa tajiri, pia suleman Mungu alimpa utajiri mkubwa sana fedha, dhahabu, mifugo na kuwa tajiri kuliko wafalme wote kwa nini?

sababu suleman aliomba hekima na maarifa , ukishakuwa na hekima uwezi kuwanyanyasa wengine, unakuwa mnyenyekevu , kusaidia wengine hivyo Mungu anakuamini na hii ndio maana watu wote waliopata utajiri kwa njia za Mungu ni watu wenye hekima na sio wajivuni au kupenda sifa , ni watu wenye kusaidia wengine kwa mipaka.

Kwa nini watu baadhi wanaokesha kusali sana kanisani awafanikiwi au maskini, kitu ambacho unatakiwa kutambua Mungu ndie aliyeleta idea ya kufanya kazi,

Mungu alipo muumba Adam alimuambia haitunze bustani ya Aden(hiyo tayari ni kazi) hivyo Mungu ubariki kile ulichonacho mkononi, Omba , kuwa na imani then fanya kazi matokeo mwachie Mungu hapo utafanikiwa.

Pia kipindi wanawaisrael wapo jangwani wanaitaji maji, Mungu alimuliza Musa una nini mkononi Musa akasema fimbo, Mungu akamuambia Musa piga mwamba , Musa alipiga maji yakatokea hivyo Mungu ili akubariki lazima uwe na kitu tayari mkononi hivyo maombi yaambatane na kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…