Wana Jamvi kuna kitu kinanichanganya kidogo nikaona ni share na nyinyi. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na idadi ya vijana kuandika vitabu. Hata hivyo kwa akili yangu ndogo naona kama ni mbeleko ya kisiasa kutoka kwa watu hao wanaoandika vitabu vyao. January Makamba alitoa kitabu cha Bumbuli akagombea Ubunge, akashinda. Sasa ameshatoa kitabu kingine, akiwa na lengo la kugombea urais.
Mwaka huu pia tumemsikia au kumuona Mbunge wa Nzega, Khamis Kigwangwallah, akitangaza kitabu chake, akiwa na lengo la kugombea Urais wa Tanzania. Siku za karibuni pia nimeona bwana anayeitwa Kambi Mbwana, naye ametoa kitabu chake kinachoitwa DIRA NA TUMAINI JIPYA HANDENI, kikiwa na maudhui kadha wa kadha.
Nilikisoma kitabu cha Makamba, najiandaa kusoma cha Kigwangwallah, lakini pia nimenunua kitabu cha DIRA NA TUMAINI JIPYA HANDENI ili kuangalia kilichomo. Hata hivyo, nashawishika kuuliza au kuamini kuwa msururu wa vitabu hivi si vya kisiasa? Kwamba ni idea nzuri kwa watu hao kujijenga kama wanazo ndoto hizo za siasa? Je, kwa kitabu kama DIRA NA TUMAINI JIPYA HANDENI, hakiwezi kuwa mwiba mkali kwa mbunge wa Handeni ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Abdallah Kigoda, ambaye duru zinaonyesha atagombea tena ubunge kwa kipindi cha tano hapo mwezi Oktoba mwaka huu kwa tiketi ya CCM.
Nawaza sana yani, duh