Ni utaratibu tu usio rasmi wa timu 'ndogo' katika ligi kuonesha bidii na maarifa mengi wachezapo na timu kubwa. Malengo yanaweza kuwa mengi, ila baadhi ni kwa wachezaji kutaka kuonekana na kusajiriwa na timu kubwa, makocha wazawa kutaka kuonekana wana uwezo kama ule wa makocha wa kigeni, nk.
Lakini pia baadhi ya timu huwa na mafungamano ya wazi au siri na timu ngingine na hivyo kuathiri mfumo mzima wa uchezaji. Mfano mdogo tu enzi timu ya Toto Afrika ya Mwanza ilipokuwa inashiriki ligi kuu, ilikuwa ni rahisi sana kufungwa na Yanga! Ila siyo Simba!
Umeelewa walau kidogo tu?