Nilishuhudia jana hali hii hapa Manispaa ya Iringa; msafara wa CHADEMA ulikuwa shwari na tulivu. Watu wao wote walikuwa katika magari na hakukuwa na umati ulikuwa ukifuata nyuma kwa miguu.
Aidha kwa mbele walikuwa na gari lao la matangazo ambalo halikuwa likirusha/ likitangaza chochote zaidi ya kupiga muziki (wimbo maarufu wa "peoples' power"). Kifupi haukuwa na tofauti na msafara wowote wa harusi.
Lakini kilichotia hofu ni idadi ya polisi wa kutuliza ghasia katika gari zao pamoja na gari ya kamanda wa polisi mkoa iliyokuwa ikifuatilia kwa nyuma.
Polisi hawa walivalia mavazi yao ya kutisha. Aidha polisi hawa waliwekwa ktk maeneo zaidi ya kule msafara wa Dr. Slaa ulikoishia. FFU walijipanga katikakati ya barabara ya eneo la Kihesa katikati ya kituo cha FFU na Majembe.
Na hili lilinifanya nijiulize, "nini hasa lengo la jeshi letu? Je, ni kweli polisi wetu, hasa kamanda wa mkoa wa Iringa hawana uelewa (hata wa kawaida tu, si lazima wasome saikolojia ya binadamu) kuwa hali hii ni kutisha wananchi? Je, si kujenga hofu? Hapa ndipo mwenye busara yoyote atajiuliza hiki kinachoimbwa "tz ni nchi ya amani na utulivu kiko wapi"
Je, huu ni uonezi au hujuma kwa vya vingine vya siasa? Mbona ni kawaida kwa ccm kupokea viongozi wao kwa maandamano?
Ninajiuliza, " nini hasa hofu ya serikali hii?
Ejl
kwa ninin