Msaada wa uhamisho unahitajika

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2018
Posts
1,152
Reaction score
3,967
MSAADA UNAHITAJIKA

Kwanza kabisa niwape pole kwa shughuli zenu za hapa na pale.

Mimi nimefanikiwa kubadilishana na Mtu wa Kaliua mkoa wa Tabora. Kwahiyo mda sio mrefu nahamia Kaliua.

Tatizo langu ni kwamba nataka kuhamia Tabora mjini japo Document zangu za kubadilishana zinanitaka niende Kaliua.

Je, kama ninataka kuhamia Tabora mjini Juu kwa juu (Kiutu uzima) natakiwa kukutana na Nani pale Tabora kuanzia Mkurugenzi, Afisa Elimu, Katibu tawala au Nani?

Shukrani.
 
Sasa huko Kaliua unataka aende nani mkuu? Huko pia kuna wanafunzi wanahitaji walimu.
 
Ulikua unafundisha wapi hadi ukaomba uhamisho wa kwenda Kaliua ndugu?
 
Andika barua uende nayo kwa Kativu tawala umuambie shida yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…