Msaada wa kufunga Wi-Fi

Naweza konect watu 10 na wao wakapata speed Ile Ile ya 10mpbs mkuu?
Ndio utaweza ku- connect hadi watu 10. Lakini speed utakayoipata haitakuwa sawa kama ambavyo ungetumia wewe mwenyewe, kwa sababu ukishaunganisha mtu zaidi ya mmoja kwenye kifaa chako cha Internet, wote mnakuwa mnagawana matumizi ya speed hiyo ya 10Mbps au 20Mpbs. Kwa lugha nyingine, speed utakayoipata itategemea na wenzako unaotumia nao wanatumiaje.
 
Ooh! Hii inautofaut Na fibe ambazo zenyewe network yake haishuki
 
Ooh! Hii inautofaut Na fibe ambazo zenyewe network yake haishuki
Zote ni sawa, iwe unatumia wireless Internet, Fiber Internet au VSAT Internet. Ukinunua 10Mbps au 20Mbps, kweli utaipata hiyo speed ya 10Mbps au 20Mbps. Lakini ukiashaongeza watumiaji, lazima kiwango cha spidi kitapungua kwako na kwa watumiaji wengine mnaotumia nao pamoja.

Ili uweze kuelewa vyema ninachozungumzia hapa, naomba nikupe mfano huu: Chukua chungwa moja zima kisha ulimenye na uliandae vyema tayari kwa kulila. Hilo chungwa ukiamua ulile wewe mwenyewe, basi utakula lote wewe mwenyewe na utaufaidi utamu wake wote wewe mwenyewe. Lakini, ukishaamua kugawana na wenzako, basi ni lazima ulikate hilo chungwa vipande vipande ili kila mtu uliyekusudia ale hilo chungwa, naye apate kipande kidogo ili naye aonje utamu wake. Vivyo hivyo hali hii ipo katika matumizi ya Internet pia. Ukiamua kutumia Internet yote wewe kama wewe bila kumuweka mtu mwingine atumie, basi utaipata speed yote ya 10Mbps au 20Mbps. Lakini ukiamua kuunganisha na wengine ili watumie hiyo Internet, basi lazima mgawane hiyo speed ya Internet ya 10Mbps au 20Mbps.
 
umeelezea vizuri sana
 
ningekupa Thanks 3 ila haiwezekani, umeelezea vizuri sana
 
Oooh Sawa mkuu nimekuelewa vzr na vip ulipiaji wake kwa mwezi ukiisha huduma inasimama na ciku ntakayo nipia tena itaanza au Kuna sheria?
 
Oooh Sawa mkuu nimekuelewa vzr na vip ulipiaji wake kwa mwezi ukiisha huduma inasimama na ciku ntakayo nipia tena itaanza au Kuna sheria?
Kuna terms na conditions ambazo utapewa siku utakayoamua kujiunga na huduma yao
 
Vip mkuu hyo wifi ya voda inachkua mda gani kumaliza process hadi kuwa wamekufungia huduma tiari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…