Msaada wa kiufundi tafadhali

kamili

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Posts
1,219
Reaction score
855
Nina matatizo mawili. Kwanza; Kwa zaidi ya mwezi sasa compyuta yangu aina ya dell ambayo nimeitumia kwa zaidi ya miaka miwili, imekuwa too slow na tena hata kufungua internate ni shida kweli. Sina mashaka na virusi kwani natumia kaerpesky ambayo ninaiapdate almost daily. Nimeiscan haikusaidia, nimetoa mafaili yote pia haikusaidia.
La pili; kutokana na shida nikawa naenda internate cafe, na moderm yangu ikapata virusi ambavyo baadae niliscan kutumia hiyo compyuta yenye shida ya uzito.
Japokuwa ilionekana virus vimeondolewa, ile flash nikiifungua sioni mafaili yake. Lakini nikiangalia space inaonesha imejaa. Halafu nikiiscan naona yale mafaili yanatajwa na antivirus kuwa yapo. Je ina maana virusi bado wapo? Na kama ndio ina maana keperskay imeshindwa? Kibaya zaidi flash hiyo niilingiza kwenye hp ambayo sijaiwekea antivirus.
Samahani kwa maelezo marefu. Naomba msaada wa mawazo.
 


kaspersky ni antirus nzuri ila inahitaj mashine yenye uwezo mkubwa kwan hata mm zaman nilitumia dell.. kaspersky huifanya computer uwezo mdogo kua slow. hvyo nakushauri u backup mashine. embu angalia speed ya mashine..
 

Umetoa maelezo marefu lakini haujaeleza kuhusu huyo mgonjwa mkuu...hatujamfahamu kabisaa inakuwa ngumu kumwandikia dosage!Btw, umejaribu kuclear temp files? Ushauri mzuri ni kubackup na kisha fanya clean installation ya windows, baadaye rejesha antivirus yako na uinstall software zako mashine itarudi poa! Kuhusu files za kweny flash zote zitakuwapo ila virus walizificha, fanya hivi:
1. Nenda Start > Run > andika cmd
2. Kisha cd\
3. Andika drive letter ya flash yako, mfano F: kisha enter
4. Andika attrib *. -h -s /s /d kisha enter
5. Andika exit kisha enter

Fungua flash yako.
 

shukrani mkuu. Kuhusu flash nimefanya kama ulivyoshauri nimefanikiwa. Asante sana. Hili la pc sijafanikiwa nadhani sijaelewa jinsi ya kufanya kwa usahihi. But usijali nimejifunza kitu.
 
Machine kuwa slow, na hasa kwa vile ishawahi kupata virus nakushauri fanya fresh installation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…