Msaada wa kitabibu kwa tatizo la vidonda vya tumbo

kubewa iddy

New Member
Jan 20, 2015
1
0
wana JF mi ninasumbuliwa na tatitzo la vidonda vya tumbo, naomba mwenye kujua suluhisho la hili tatizo kitabibu zaidi anipe msaada wake maana nateseka sana
 
wana JF mi ninasumbuliwa na tatitzo la vidonda vya tumbo, naomba mwenye kujua suluhisho la hili tatizo kitabibu zaidi anipe msaada wake maana nateseka sana
Jipige ununue juicer mashine ya maana hata pale game mlimani zipo. Tengeneza juisi ya kabeji kila siku asubuhi na unywe kwa muda siku kumi mpka kumi na nne mfufulizo. Kunywa hiyo juisi saa moja kabla ya kutia kitu kingine tumboni.

Binafsi niliteseka na vidonda vya tumbo kwa zaidi ya miaka minne na madawa ya hospitali hayakusaidia kabisa.

Nilipewa hiyo tiba na ndani ya wiki tu niliona mabadiliko makubwa na nimepona kabisa maharage na pilipili nakula kama kawa.

Muhimu ninachokuomba ni kuleta mrejesho tu humu. Kusaidiana muhimu. Ubarikiwe
 
Jipige ununue juicer mashine ya maana hata pale game mlimani zipo. Tengeneza juisi ya kabeji kila siku asubuhi na unywe kwa muda siku kumi mpka kumi na nne mfufulizo. Kunywa hiyo juisi saa moja kabla ya kutia kitu kingine tumboni...
Juice ya kabeji ndio juice ya kabichi? Na kama jibu ndio naitengeneza vipi?
 
wana JF mi ninasumbuliwa na tatitzo la vidonda vya tumbo, naomba mwenye kujua suluhisho la hili tatizo kitabibu zaidi anipe msaada wake maana nateseka sana

Ulifanya vipimo gani ili kuthibitisha kuwa una vidonda vya tumbo !?

Tafiti zimeonyesha kuwa tatizo la vidonda vya tumbo vinasababishwa na aina ya bacteria wajulkanao kama HELICOBACTER PYLORI.

Hivyo mbali ya dalili nyinginezo anazokuwa nazo mtu kipimo hiki ni muhimu ili kuthibitisha uwepo wa tatizo husika.

Na pindi unapogundulika kuwa na aina hiyo ya Bacteria utapewa mchamganyiko wa dawa kwa ajili ya kukabliana nao. Hii itasaidia kutoa nafasi ya vidonda kupona/healing process ikiwa ni pamoja na kufuata masharti na ushauri wa kitabibu ilikupata matokeo chanya.
Iwapo utaonekana kutokuwa na Bacteria hao uchunguzi zaidi utafanyika kujua kiini cha tatizo.

Mfano unaweza kuwa na tatizo la mwili kuzalisha kwa wingi asidi (GAstric ACID) tumboni kuliko inavyotakikana. Vivyo hivyo matatizo ya umengenywaji wa chakula yanaweza kusababisha mwili kuwa na GESI nyingi inayoweza kupelekea maumivu ya kuchoma kama mtu mwenye vidonda.

Hivyo aina ya tiba/tiba sahihi itategemea usahihi wa ugunduzi wa kiini cha tatizo.
 
Ulifanya vipimo gani ili kuthibitisha kuwa una vidonda vya tumbo !?

Tafiti zimeonyesha kuwa tatizo la vidonda vya tumbo vinasababishwa na aina ya bacteria wajulkanao kama HELICOBACTER PYLORI.
Hivyo mbali ya dalili nyinginezo anazokuwa nazo mtu kipimo hiki ni muhimu ili kuthibitisha uwepo wa tatizo husika.
Na pindi unapogundulika kuwa na aina hiyo ya Bacteria utapewa mchamganyiko wa dawa kwa ajili ya kukabliana nao. Hii itasaidia kutoa nafasi ya vidonda kupona/healing process ikiwa ni pamoja na kufuata masharti na ushauri wa kitabibu ilikupata matokeo chanya.
Iwapo utaonekana kutokuwa na Bacteria hao uchunguzi zaidi utafanyika kujua kiini cha tatizo. Mfano unaweza kuwa na tatizo la mwili kuzalisha kwa wingi asidi (GAstric ACID) tumboni kuliko inavyotakikana. Vivyo hivyo matatizo ya umengenywaji wa chakula yanaweza kusababisha mwili kuwa na GESI nyingi inayoweza kupelekea maumivu ya kuchoma kama mtu mwenye vidonda.

Hivyo aina ya tiba/tiba sahihi itategemea usahihi wa ugunduzi wa kiini cha tatizo.
good.

je matatizo ya vidonda yanaweza sababishwa na sababu zote mbili kwa pamoja kama ulivyo taja hapo juu? yaani bacteria na asidi kuzidi?
 
wana JF mi ninasumbuliwa na tatitzo la vidonda vya tumbo, naomba mwenye kujua suluhisho la hili tatizo kitabibu zaidi anipe msaada wake maana nateseka sana
Pole sana mie nilikua mhanga wa hili tatizo nashukuru Mungu kwa sasa naendelea vyema, jambo la msingi katika kupona na kutibu vidonda vya tumbo sio kukimbilia kula madawa kikubwa badili mfumo wa maisha unaoishi hasa kwa kuangalia unakula/kunywa nini na kwa wakati gani.
Ukiweza zingatia lishe vizuri unaweza pona kabisa bila hata kutumia dawa yoyote hasa kwa wale waliokatika hatua za awali.
 
Jitahidi kupata mchemsho wa bamia au juice yake km utaweza. Pia jitahidi kula mboga ya mlenda vimenisaidia sana hivyo.
 
Jipige ununue juicer mashine ya maana hata pale game mlimani zipo. Tengeneza juisi ya kabeji kila siku asubuhi na unywe kwa muda siku kumi mpka kumi na nne mfufulizo. Kunywa hiyo juisi saa moja kabla ya kutia kitu kingine tumboni.
Binafsi niliteseka na vidonda vya tumbo kwa zaidi ya miaka minne na madawa ya hospitali hayakusaidia kabisa. Nilipewa hiyo tiba na ndani ya wiki tu niliona mabadiliko makubwa na nimepona kabisa maharage na pilipili nakula kama kawa.
Muhimu ninachokuomba ni kuleta mrejesho tu humu. Kusaidiana muhimu. Ubarikiwe
Ahsante kwa kuwa wazi.
Kitu kingine ambacho nimekitumia na kimemsaidia my wife ni majani ya mlongelonge .. amepona kabisa.
 
Back
Top Bottom