Msaada tiba ya jino

Habari ya muda huu wana jf, nasumbuliwa sana na jino, limeshambuliwa na wadudu....kuna yeyote mwenye kufahamu tiba yake bila kung'oa
Ntakuwa Dar baada ya siku nne. Kama utakuwa hujapata dawa utanitafuta nikupe dawa, tena bure.
 
Asante,hii ni ya kutunza kwa baadae
 
Habari ya muda huu wana jf, nasumbuliwa sana na jino, limeshambuliwa na wadudu....kuna yeyote mwenye kufahamu tiba yake bila kung'oa
Pata maganda ya mti wa Mlonge. Pondaponda na yachemshe (kama kikombe kimoja hivi). Sukutua kama unavyofanya wakati wa kubrashi meno. Unaweza kufanya asubuhi, mchana na jioni kwa siku tatu. Halafu nipe mrejesho.
 
Kwa ninavojua issue ya jino dawa huwa ni kung'oa tu, nyingine labda useme dawa ya kutuliza maumivu tu kwa muda.
 
Mkenda jengo la ubungo plaza uliza duka la dwa za asili la JKBC waambie wakupe dawa ya meno inaitwa DFP inauzwa Kati ya elfu 20 Hadi 25 utanikumbuka baadaye.
Kwa Dodoma wapi inaweza patikana?
 
Wadau nimerudi kwenye huu uzi kuwapa mrejesho, mlinipa msaada mkubwa sana, kila mmoja kwa kile alichoona kingenisaidia niwashukuru sana wote...binafsi niliamua kutumia ile njia niliyoona ina wepesi, basi niliamua kutumia dawa ya sensodyne kama ambavyo mmoja wa wana jf alivyoshauri hapa na mmoja wa wana jf.kwa kweli dawa ile iko vizuri sana...meno yametulia kabisa...kuanzia sasa sitoacha hiyo dawa...na ningependa niwashauri na wengine watumie dawa hii kama utaratibu wao wa kawaida kila siku kwa kuswakia asubuhi na usiku/jioni.
 
Ya ndulele umeiacha mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…