google ilipoenda hewani ndio ulikuwa mwisho wa kuuliza, muda uliotumia kuandika hiyo paragraph, ungegugo tayari ungekuwa na majibu ya kesi yako.
Heshima kwenu nduguzangu
Samahani najua hapa kuna wadau wa mambo ya IT na mambo mengine mazuri
Nina PC yangu ni ASUS ina HDD 250, PROCESSOR@ 1.67, 32-BIT OPERATING SYSTEM, na RAM ya IGB, nimeitumia kama mwaka sasa, sasa kwa siku za hivi karibuni imekuwa slow sana, niimehangaika kuulizia ulizia kwa jamaa wananiambia lazima ninunue RAM nyingine yakuanzia 2GB na kuendelea,
Nimeona kabla ya kufika kununua RAM mpya etc, nikaona niulize wadau hapa JF (KISIMA CHA MAALIFA) kama mnaweza nisaidia kupata labda software kama zipo za kuboost pc, maana sometime hata kuzima inachelewa kidogo, kufungua mafaili inasikilizia sana, na uki fanya komandi kama 3 hivi kwa haraka haraka pasi ndio inachanganyikiwa kabisa.
Msaada tafadhaili
Cc. C6, Fadhili Paulo, sijui nini,ejoka, chief-mkwawa... et al
sijui nitakuwa sahihi, maana si mtaalamu sana wa pc, but nimecheki katika properties za computer inaniambia ni windows 7 starter.. sasa sijui ndio ulihokua unataka mkuu??
Mimi mwenyewe na tatizo kama hilo. Natumia w7 home basics, pc ni dell insipiron min, ram 1 gb, processor 1.67 ghz, hdd 229 gb, ant- virus avast. Naombeni msaada wenu.
Kama unatumia windows xp basi jaribu hii HAPA, mimi naitumia siku zote na pc haisumbuwi, ina mode 2 Simplified na Expert, kwa mara ya kwanza i-run katika expert mode, pia niambie unatumia antivirus na firewall gani nikusaidie zaidi.
Avast inatumika na watu wengi sana duniani ila inataka uwe unai-update kila mara, nakushauri utumie na ile internet security yao. Lakini kitu kingine kibaya kwa avast ni ule ukubwa wake, ni kubwa avast nadhani ni zaidi ya mb 200 kwa sasa na inalazimisha iwepo kwenye start up programs. Fanya usafi wa pc yako kwa kutumia hiyo software hapo juu na ulete feedback