Nelson muna
New Member
- Jul 28, 2015
- 4
- 10
Habari wadau , Nina gari yenye engine ya 1zz ina tatizo la engine kutetemeka na rough idle sana sana ikiwa silence au slow speed, pia exhaust ina tetemeka mpaka inagusana na body.
Nilienda kwa fundi akafanya;
1. Kusafisha fuel filter.
2. kubadili spurk plug
3. kusafisha nozzle.
4. kubadilsha engine mount moja iliyokufa.
Badaa ya hayo marekebisho vibration imepungua tu lakn bado shida iko pale pale.
Note:
1.Exhaust nilibadilisha baada ya wahuni kukomba catalyst converter.
2. Plug nimefunga k16R-u11 sina uhakika kama ni genuine.
3. Hakuna kiashiria chochote kwenye dashboard kama kuna shida.
Je, kuna shida gani naomba ushauri.
Asante
Hiyo ni Ignition Coil
Cheki zote ukiweza badilisha
Asante kwa ushauri, Lakini ignition coil walizicheki hazina shida.Hiyo ni Ignition Coil
Cheki zote ukiweza badilisha
Bwana Mkubwa heshima yako.1zz ni cylinder 4. Kama ingekuwa misi ya coil isingekuwa inatokea tu kwenye sailensa au low speed.
Kuna leakage bila shaka hata mie napata hilo tatizo kwa sasa! Mwanzo maji yalikuwa yapo level tu yani ukifungua mfuniko tu unayaona!Bwana Mkubwa heshima yako.
Naomba Uelewa tu japo haihusini kabisa na Topic hii.
Naomba kujua Maji kwenye gari ya Kupoza injini, Je yanatakiwa yaonekane kwa Macho unapofungua tu Mfuniko yaani yawe Juu kabisa Pomoni ama nitajuaje yamo?
Nina kagari kangu naona muda wote sioni Maji Juu, nikijaza Mpaka Juu, kesho nachek nakuta hayaonekani, naongeza tena.
Sasa najiuliza ni Leakage au Normal kwa kutojua tu.
Pia Maji kidogo yanavujia kwa Juu Mfuniko gari ikiwashwa, kwa muda tena yanakata yana rangi kama ya Kijani yanapotoka ila ukigusa na Kuangalia Mkononi unaona tena hayana rangi.
Tafadhali Mtaalam ufahamu kwenye hilo. Ahsante.
Nimekupata Mkuu, inabidi Kuifanyia kazi hii.Kuna leakage bila shaka hata mie napata hilo tatizo kwa sasa! Mwanzo maji yalikuwa yapo level tu yani ukifungua mfuniko tu unayaona!
Na ukitaka kuamini hilo anza ku monitor reservior ya maji! Ikianza kupoteza maji kila siku inakuwa empty jua kuna mahali maji yana leak!
Mie nilibadilisha cover la pembeni la rejeta tatizo limeisha.Nimekupata Mkuu, inabidi Kuifanyia kazi hii.
Cover ipi mkuuMie nilibadilisha cover la pembeni la rejeta tatizo limeisha.