Msaada: Nikila nahisi kama joto tumboni, tatizo nini?

Mpigadili Tz

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,076
1,957
Habari zenu, kuna wakati nikila kitu huwa nahisi kama joto tumboni hata kama maji ya baridi japo sio mara zote ni mara chache sana hii husababishwa na nini?
 
Unapokula mfano vyakula gani mbali na maji.....jaribu kwenda hospital unaweza kuwa na vidonda vya tumbo
 
Kumbe wa kiume? Acha kula maharage na kutumia pilpil inaweza ikawa vidonda vya tumbo!
Weka vizuri mkuu kua kama ana vidonda vya tumbo asitumie maharage na pilipili
Asije akafikiri umemwambia maharage yanasababisha vidonda vya tumbo
 
Unapokula mfano vyakula gani mbali na maji.....jaribu kwenda hospital unaweza kuwa na vidonda vya tumbo
Huwa inatokea nikikaa mda mrefu bila kula ndo inatokea hali hiyo mfano nisipokula mchana alafu usiku nikila ndo hutokea na vyakula ni hata ugali
 
Huwa inatokea nikikaa mda mrefu bila kula ndo inatokea hali hiyo mfano nisipokula mchana alafu usiku nikila ndo hutokea na vyakula ni hata ugali
Hizo ni dalili za vidonda vya tumbo, hakikisha hukai na njaa kwa muda mrefu, vile vile kama ni mtumiaji wa pilipili acha mara moja na hakikisha unaenda hospitali haraka. Pia njaa nayo inasababisha tumbo kuwa moto.
 
Back
Top Bottom