Kwanza ni vizuri ukachunguzwa afya yako vizuri kwa sababu vinahusiana na HIV infection. Pili tiba yake inategemea ni vingi kiasi gani. Inategemea na wingi wake, vyaweza tibika na hiyo caustic pensil, au Podophylline au kama ni vingi sana hufanyiwa cauterization hospitalini.
Kama unatumia caustic pensil, naamini utakuwa umeelekezwa tahadhari ya jinsi ya kutumia. Baada ya kuchukua tahadhari hizo hakikisha ile caustic pensil unaituliza kwa dakika tatu kwa kila kimelea cha warts. Kwa hiyo baada ya kutuliza hiyo caustic pensil kwenye kimelea kimoja unahamisha kwenye kingine nacho unakichoma kwa muda huo mpaka vyote vimeisha. ukifanya hivyo huwa havirudi na vikirudi huwa ni vichache sana ukilinganisha na vya mwanzo, na hivyo ukirudia huwa vinaisha kabisa.
Pili mkague patner wako kwa sababu vinaambukiza, ili nae apate tiba.