Matumizi ya gari ni yapi, utalitumia kila siku? au mara chache kwa wiki? unataka gari inayotumia mafuta kidogo? una familia au uko mwenyewe? gari litatembea barabara nzuri au mara nyingi litatembelea barabara ya vumbi? ni gari lako la kwanza? au tayari ushamiliki mengine? je unahitaji gari ambalo ukitaka kuuza hutosumbuka? ukiwa umejiuliza maswali haya na mengine automatically utajua ununue gari gani! lakini kwa bajeti hiyo ukitaka gari zuri lisilosumbua agiza japan kwenye kampuni za kueleweka kama trust, sbt, autocom na mengine, pili nunua ukoo wa toyota, tatu nunua la cc 1300-1500 hapa utapata toyota raum, ist, auris, rumion, axio na mengine mengi tu.