WA MAMNDENII
JF-Expert Member
- Jun 5, 2010
- 344
- 58
mchunguze ana kipaji gani Mungu hakunyimi vyote endeleza kipaji chake kiwe ajira yake
Much thanks mkuu kwa ushauriMuulize akiwa yuko free kabisa nayuko hepi kwamba anataka afanye kazi gani ? Utashangaa atakavyofanya vizuri kwenye hiyo kozi.
Kuna mwanzilishi wa kiwanda cha pikipiki Japan alikua hivyo hivyo, ila babake alipomuuliza nakuambiwa dogo ana interest ya ufundi wa pikipiki, dogo alifanya ufundi mpaka akafungua kiwanda. Hata akikuambia anataka kufuga nguruwe usimcheke. Muendeleze huko huko anakotaka
Mimi nina mambo mawili ya kuchangia katika mada hii.
1. Mdogo wangu anayenifuatia alionekana kuwa ana uwezo mdogo darasani. Japo sikwa kiwango hicho unachosema. Nilimrudisha nyuma madarasa na nikawa namtafutia shule nzuri na walimu wa tuition. Akiwa form three mwalimu wake wa tuition akanieleza kwamba niache kabisa kumsomesha nimnunulie gari ndogo afanye biashara ya taxi. Sikuchukua ushauri wake, badala yake niliendelea kumpa encouragement na support. Chuo nilimchagulia BA ambayo nilijua. Hivi sasa yeye ni meneja ofisi flani.
2. Last born wangu akiwa nursery school mpaka standard one, walimu walisema uwezo wake mdogo mno. Kipindi flani nilimuandaa mwenyewe for class tests, alifaulu sana. Nikajua anao uwezo. Akiwa standard 2 tukahamia nchi moja za magharibi. Huku nako walimu hawa wazungu wakasema ana uelewa mdogo. Wakamuandalia wataalam wa child psychology. Costs zote ni kwa serikali. Wakampa mpaka laptop humo waka install programs nyingi za kuinua iq. Hivi sasa anaperform vizuri sana. Lakini principal wa shule alinambia neno moja. Alisema mwanangu hana tatizo ila tumchukulie kama an individual na tumpe support ya kumtia moyo.
3. Nilisoma primary na mtoto mmoja ambaye uelewa wake ulikuwa chini sana. Wazazi wake walijaribu kumrudisha nyuma. Hata sekondari nahisi kuna namna walivyofanya ili itangazwe kafaulu. Ukumbuke huko nyuma tulikuwa na sekondari chache tz. Alipofika form four ikashindikana kabisa. Bado hawakukata tamaa. Walimpeleka kozi za hotel management. Sisi tuliona kwamba huyo kafeli maisha. Hivi sasa yupo state moja USA ni meneja wa hotel.
4 Mwisho, kama wewe ni mkiristo, fanya kila mara hiki nilichofanya na bado nafanya kwa wanangu. Muombee wewe mwenyewe mwanao. Siyo lazima kumwekea mikono, ila huwe una mbariki mwanao kwamba awe na ufahamu mzuri darasani na awe na future nzuri. Sisi wababa tuna power kubwa sana kiroho kwa watoto wetu na kwa mke wetu pia. Kristo ni kichwa cha mume. Mume ni kichwa cha familia. Sikushauri kumpeleka kwenye vituo vya maombi maana hakuna atakaye weza kumuombea kila mara na kwa miezi mingi. Fanya wewe kama umebatizwa. Kila mkiristo aliyebatizwa anao uwezo wa kufungua yaliyofungwa kwa njia ya sala. Mhudumu mmoja USA anaitwa Francis Mcnutt alitunga kitabu kinaitwa Soaking Prayer. Kinakushauri kwamba kama unaona tatizo ni kubwa basi liwekee ratiba ya sala tena fanya hivyo kwa miezi au miaka.Usiweke imani yako kwa wachungaji hao nao wana matatizo yao na wengi wao ni wajasiriamali.
Asante
Mungu akunyimi vyote, mimi nina dogo hapa nyumbani, wenzake alioanza nao std one sa hv wapo form two yeye ndo yupo la saba, yani kichwani zero kabisaaaaa,! Ila sasa ana utundu wa mambo ya electronics, ukiingia chumban kwake kama umeingia TANESCO yan anaweza akatengeneza kitu cha umeme mpk unabaki unashangaa,alishawahi kutengeneza tv mpk ikafanya kazi, sema mfumo wetu wa elimu ya tanzania ni mbovu, wenzetu huko wakiona anakipaji flani, yan huyo wanamchukua fasta wanamwendeleza na kipaji chake,! Kikubwa ukae nae chini then umuulize kitu gan anakipenda.
Sijalisoma neno la mwisho chiefHakuna kitu kama "slow learner"
Huyo mtoto anatatizo la ku lose concentration,kutokuwa focused
Mambo ya kumbukumbu yanakuja with practice.Kuna mental exercise za kuongeza memory ka mnemonics