Msaada: Matatizo ya masikio

Fohadi

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2020
Posts
774
Reaction score
2,439
Habari zenu wakuu,

Kiufupi sina historia ya kuwa na matatizo ya masikio na wala sio mtumiaji/ mpenzi wa earphones. Mabadiliko katika masikio yangu nimeanza kuyaona ndani ya kipindi cha miezi miwili iliyopita. Hii hali imekuwa inakuja na kupotea ila kwa hizi weeks 2 imekaa muda mrefu. Iko hivi;

Masikio yanasikia vizuri ila kuna hali fulani strange naiona kwenye masikio yangu. Hali ninayoipata ni kama anayoipata yule mtu aliyekaaa jirani na speakers za mziki mkubwa kwa muda mrefu akitoka hapo lazima kuna sauti fulani kama ya muungurumo au filimbi ambayo atakuwa anaisikia ndani ya masikio yake...sasa kwangu mimi hii ndiyo hali ninayokuana nayo..inaenda mpaka nafikia muda naona kabisa napata maumivu ndani ya masikio..

Nimetumia dawa aina ya BORIC ACID lakini hadi sasa bado sijaona mabadiliko. Ningependa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu je tatizo linaweza kuwa nini na ni dawa ipi nzuri inayoweza kunisaidia maana kuna muda natamani hata kuyaziba masikio kwa mikono ili kupunguza ile hali ya kelele na maumivu niipatayo.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Mkuu pole sana kwa hayo maradhi yako uliyo nayo. Una maradhi kwa jina la kitalam wanayaita (tinnitus) Muungurumo ndani ya masikio hiyo inatokana kwakutumia vidonge vya kutuliza maumivu ya mwili au maumivu ya kichwa kwa wingi ndio imekusababisha upatwe na hayo maradhi . Kwa Dawa za Hospitali utatumia na kubadilisha kila ya aina ya dawa sio rahisi kupona maradhi yako.




Can tinnitus be cured naturally?
There is no cure for tinnitus. However, it can be temporary or persistant, mild or severe, gradual or instant. The goal of treatment is to help you manage your perception of the sound in your head.

There are many treatments available that can help reduce the perceived intensity of tinnitus, as well as its omnipresence. Nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kukutibia kwa dawa zangu na uweze kupata maradhi yako uguwa pole.
 
Kwahio maradhi yake yataponaje sasa?kuna dawa mbadala au ndio aishi nayo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…