Msaada: Masikio yananitesa sana, nimechoka kuchekwa na kudharauriwa

Kama wewe ndio unayeongoza mada, nini kinakukatisha tamaa wakati hadhira itakuwa inakusikiliza? Ingekuwa mtu mwingine anaongea, hapo ungekuwa na wasiwasi wa uwezekano wa kutomsikia vizuri.
Jiamini, na hakikisha unamaliza masomo yako.
 
Achana nao piga shule wajinga darasani ndo huwa wanawacheka wenzao ili wao waonekane bora
 
Usiache, fanya mitihani.

Ukiquit kufanya mitihani leo kesho utaquit nini? Kesho kutwa utaquit nini?

Katika presentation wengi tunachekwa. Na tunasikia.

Kuquit leo itakua umeweka alama ya jinsi utakavyopambana na changamoto katika maisha yako.

Fanya mitihani.
 
First huduma ya afya imetanuka sana Tanzania, nenda hospital inawezekana kuna tiba itakusaidia.

Second, dawa ya bishoo ni kuwa bishoo zaidi yao, so pamabana mambo yako yawe mazuri mbeleni waje kukuomba kazi then uwaajiri kwa mbwembwe na kuwatumikisha kama punda.

Lastly, asilo na hili ana lile, kila mtu anaudhaifu wake, wewe wako unaonekama wa wengine unaweza usiwe unaonekana, so no worries, mungu hakukosea kikuomba hivo, anasababu kamili ya kukifanya kuwa hivo, just do your best na utaona mambo yako yanafunguka huko mbeleni.
 
ushauri
Kuchekwa kila mtu anachekwa ni vile wewe unachekwa tu kwa sauti. Kuchekwa ni mbinu yakukutoa mchezoni sasa kama unataka kutoka mchezoni ni maamuzi yako, na ukifanya hivyo viicheko vyao ndio vitamake sense. Huwezi mjibu kila mtu au kumsikiliza kila mtu focus kwnye malengo yako piga A+, alafu waache matokeo yawacheke wenyewe. Wakipata Miswaki watajua hawajui.
NOTE
Nenda hospitali vipo vifaa vyakuongeza uwezo wakusikia.
 
Inapasa kujikubali, kwa msaada zaidi unaweza kusoma kitabu kimoja iv mimi kimenisaidia sana cos nilikuwa na matatizo mengi ambayo yalifanya niwe najishtukia mwenyewe, page zipo 100 tu

The subtle art of not giving a https://jamii.app/JFUserGuide 👇
 

Attachments

  • The+Subtle+Art+of+Not+Giving+a+F+ck+-+Mark+Manson.pdf
    911.4 KB · Views: 4

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…