Waende mahakamani wakiwa na muhtasari wa kikao Cha familia ambacho kitamteua msimamizi wa mirathi na kuainisha warithi wa marehemu, lakini pia Kama Kuna wosia wowote wa marehemu wataenda nao, wahakikishe wamepata cheti Cha kifo kutoka RITA. Mahakamani watafungua shauri la mirathi Kisha litasikilizwa na msimamizi wa mirathi atapewa utaratibu wa kwenda mamlaka husika Kama bank, nssf, n.k kufuatilia haki za marehemu na kuzigawa kwa wahusika wa mirathi Kama familia ilivyoamua au Kama wosia unavyosema...