


usiogope. Ntakueleza kutokana na experience ya kuzalisha wamama wengi. Mengi ya haya ni ya kibinadamu na maelezo ya wengi wao.
1. Asikudanganye mtu, uchungu unauma na unauma kwelikweli. Jitahidi kufanya mazoez ya kutembea ili at least kutanua nyonga.
2. Siku uchungu ukifika, ujue utakushika almost masaa 8 au zaidi lakini unaanza kidogokidogo af unazidia mida unavokaribia
3. Jitahidi uende haja kubwa wakati uchungu bado haujashika sana. Hii ni kwa sababu asilimia 90 lazma ukate nyengo wakati wa kusukuma, so ukipunguza mbolea before muda wa kusukuma utapunguza maneno ya shombo kutoka kwa wauguzi hasa wa kike. Usijefika pale ukashusha mbolea heavy ukaharibu mazingira.
4. Personaly nashauri kuvumilia maumiv na kutopiga makelele ya kiwaki maana ukishamaliza utaanza kuona aibu bkoz kila mtu atakua anakushangaa ulivokua unalia lia kwa masauti. So gugumia if you can.
5. Muda wa kusukuma ukifika, hutaambiwa, we mwenyewe utaanza kusukuma, na hapo ndo utajua maana ya maumivu. Lakini jitahidi usukume bila kuacha acha ili usije ukambonyeza mtoto kichwa.
6. Najua ni ngumu, lakini jitahidi uwe mstaarabu hasa kwenye maelekezo utayopewa na wanaokuzalisha. Hua hatupendi mtu anaejifanya much know. Ukijifanya mjuaji sana utaishia kugombana na kutopewa huduma nzuri.
7. Ukipata bahati ya kuzalishwa na mwanaume utaenjoy maana sisi kwa kias kikubwa hua tuna huruma. Hata wanawake wako pia wenye roho nzuri af kuna wale wapashkuna.
8. Andaa nguo za kutosha. Usafi ni muhimu sana kila hatua ya hiyo siku.
9. Kila la kheri. Kuzaa ni jambo la baraka, ukishajifungua ukabeba mtoto/watoto wako ukaanza kunyonyesha, furaha yake ni kubwa sana na utasahau haya maumivu yote ulopitia.
10. Muombe Mungu sana ujifungue bila complication na mtoto asipate tatizo. Lishe ni muhim after kujifungua na hakikisha mtoto ananyonya maziwa yako kwa wingi.
11. Be humble. Ukishajifungua utakutana na watu ambao hawajajaaaliwa mtoto, usiwaoshee kana kwamba wewe ndo umehangaika saana au unajua saana kuzaa, kistaarabu tu. Unyenyekevu ni kitu muhim. Oh, pia sio kila mtu ahikeshike mwanao, kaa chonjo, watu wengine sio wema.