Habari zenu wana jamii?
Naombeni mnisaidie mawazo, nina jamaa yangu mmoja alikuwa akifanya kazi katika kampuni flani hapa mjini (DSM) zaidi ya miaka 10. Ila ameacha kazi na hakuwa kwenye good terms na mwajiri wake wakati anaacha kazi hakupewa barua ya kuachishwa kazi. Anahitaji kufatilia mafao yake ya nssf. Je ni taratibu (procedures) gani anatakiwa azifuate ili alipwe mafao yake? na afanye nini endapo aliyekuwa mwajiri wake atagoma kumsainia papers zinazomthibitisha kuwa alikuwa mwajiriwa katika hiyo kampuni.? Mawazo yenu ni muhimu hapa.
Binafsi kuna mtu namfahamu yalimkuta kama hayo!!
Ukweli jamaa walimwekea ngumu ile mbaya, yaani mwajiri na nssf pia, pesa zenyewe anazodai ni ndogo za mbuzi tu, lakini zilimtesa sana kwa kipindi kifupi!!
Alifanya hv:
1. alienda pale mediation karibu na akiba, akawaeleza abc
2. wakampa barua ya kumuita pale ofcn, akakataa kuja kama mara mbili hv
3. wakamwandikia barua ya kumwita tena, akaja
4. wakaongea weeeeee lakn mwisho wa siku jamaa akatoa barua, tena na vihela kidogo kama compensation. Ila sina uhakika kama case yako imefanana sana na hii
5. baada ya hapo akapeleka barua ya kuacha kazi pale nssf temeke
6. akapewa form ya kwenda kujaza, nadhani zipo tatu hv, kuna sehemu ya kusaini mwajiri, mbunge,serikali za mitaa, nk yeye alisainishwa na serikali za mitaa
7. within three weeks za kupigwa tarehe kachukua mzigo wake kam 2.9m hv, ni nov mwaka jana
8. sijui alihonga baada ya kupewa mzigo wake, ama chuma ulete ama lah, but sasa hv najua zimeisha, zimefanya kazi ya kujenga taifa, mfumuko wa bei balaa mbaya!!
7. sasa hv maisha yake yanaendelea kama kawaida, ameshakula jasho lake!!
Mpe pole sana, but atashinda asiwe na hofu!!