LIGEDENGE 1
Senior Member
- Nov 15, 2013
- 184
- 29
Piga 100
ina lipa kaka komaaa kamtaji ka 2m kanatosha kuzungusha
@lige; line ya wakala wa mpesa yenye jina lako unaweza kupata ofisi za vodashop au super dealers, kiutaratibu ukipeleka maombi yako itakubidi usubiri kwa miezi isiyopungua mitatu ndio upate line yako, ni bure kabisa. Faida ya biashara hii ni commision kulingana na wingi wa miamala unayofanya, kadri unavyohudumia wateja wengi ndio faida inakua kubwa zaidi. Hasara yaweza kutokea kutokana na kukosekana umakini ktk huduma, wizi, utapeli n.k. Ila ni biashara nzuri sana na inalipa mno ukiwa sehemu yenye wateja wengi.
tanya mambo ya halali ndugu.wakati mwingine njia za mkato huleta majanga baadae
Kupata til nafikiri wiki tatu tu sidhani kama miezi mitatu na mtaji wa kuanzia ni 1 mill ila unaweza kuongeza kiwango chochote kuzungusha mtaji wako faida inatokana na muamala wako unaoto mzunguko ukiwa mkubwa na faida kubwa haina kukopwa hiyo kama biashara zingie
Kupata line ya M-Pesa (TILL) unaweza muona superdealer,wakala mkuu kama unamfahamu au kama uko dar-es Salaam unaweza ukafika pale makao makuu yao kitengo cha mawakala ukiwa na copy ya kitambulisho chako,copy ya TIN ya biashara na copy ya lessen ya biashara.
Muda wa kusubiri sio chini ya wiki tatu na sio zaidi ya wiki tatu.
TILL inatolewa bure na sio kwa kulipia.
Ukiuziwa TILL utapatiwa iliyokuwa ibatumika. Ambayo baadaye inaweza kuletea matatizo.
Faida inategemea na mtaji wako na eneo ulilopo. Faida unaipata kwa commission. Kila transaction inakiwango chake. So mwisho wa mwezi zijumlishwa na kupatiwa commission yako kutoka head office au wakala wako mkuu.
Hasara yake inategemea na umakini wa atakayekuwa anakusaidia kufanya hiyo shughuli. Kuna wizi mkubwa kwa upande wa mawakala unaoshamiri kila siku so ni kuwa makini na kila mteja atakaye kuja.
Kuwa makini kurecord kila muamala unaoufanya ili kuweka records.
Ni biashara nzuri ukiwa makini,thanks a lot