Msaada: Kazi za migodini

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,757
Reaction score
105,020
Habari.
Wakuu, nimegundua kwamba kazi nyingi za migodini hazitangazwi kwenye media, ata kama kunahuitaji. Zipo zinazobandikwa tu kwenye mageti ya Migodi, Notice Bord zao au nyingine wanazijua tu wafanyakazi wa huo mgodi.
Naamini JF kuna wakazi wengi tu kuzunguka migodi, wengine wafanyakazi au wengine wanajuana na wafanyakazi wa humo.

Kijana wenu nina degree ya BSc Geology, nimegraduate mwaka jana (June 2013), mwenye uwezo wa kunipigia pande maeneo hayo nipate kazi msaada please. Naweza fit kama geologist migodini ata katika exploration companies au hydrogeologist katika makampuni ya uchimbaji wa visima vya maji (au survey ya under ground water). Experience kidogo katika hii fani, nimeipatia niliko fanyia field (miezi miwili) na intern kama hydrogeologist (volunteer). Reason ya Ku-quit intern: nawaongezea sana gharama wazazi, coz per day nauli kama 2800 hivi.

Kusubiri kazi za fani hii zitangazwe ni kama kusubiri Boat Air Port. STAMICO walitangaza ila walichukua vijana wenye experience tu, Wizara ya Maji na Wizara ya Nishati na Madini wametusahau kabisa, GST nao wanatangaza kazi za masecretary na wahasibu tu, hao TPDC janga la Taifa. Nimejaribu sana kurusha jiwe gizani, kwa ku-apply kazi zisizotangazwa, ila response yao ni F au wengine "tutawasiliana na wewe tukiwa na uhitaji".

Mwenye msaada wa tatizo langu kwa kunipa opportunity au ushauri, nipo available PM au hapa hapa jukwaani wakuu.

Thanks.
 

pole kaka,kazi zimekuwa ngumu saNA siku hizi..ni za kujuana..omba mungu atakusaidia one day yes
 
Ni kweli uwa kazi nyingi za mining zinakuwa internal advertisiment,lkn ukiwa km mtaalamu wa geology ni vzr ukaingia kwny website zao.kuna sehemu ya carriers,kuna sehemu unaweza ku-upload cv na kuwa member pia kupata notification zote za kazi kupitia email yako.
 

Wazo zuri mkuu. Nimejaribu kwa web chache hasa zile majina makubwa maana wao ndio wana hiyo option. Shukrani.
 
kaza buti mkuu mwishoni wataachia, fresh from school wote 2nakumbwa na tatizo hilo haijalishi umesoma fied gani ukitoa field zinazosubili post kutoka government(i.e.ualimu,madaktari n.k.).
 
kaza buti mkuu mwishoni wataachia, fresh from school wote 2nakumbwa na tatizo hilo haijalishi umesoma fied gani ukitoa field zinazosubili post kutoka government(i.e.ualimu,madaktari n.k.).

Ilo neno mkuu. Vitu ambayo tunapaswa kutokata tamaa ni hivi:
-Kuendelea kutuma applications sehemu mbalimbali.
-Maombi muhimu sana mkuu.
-Kua karibu na matangazo (internet, magazeti etc)
-Pia wasiliana na graduates wenzio aisee.

PS: Mie vyote hivi navifanya ila nadhani muda bado.
 
ni shida kwa kweli, mi nilijua hao wa science wana uafadhali kumbe hamna kitu. nina mshikaji wangu amemaliza computer science katafuta kazi mpaka ameamua kwenda jeshini tu

Uko sahihi mkuu. % kubwa ya professionals huku Tanzania zinachukuliwa na watu wasio na sifa husika. Ndio maana graduates wenye hizo sifa wanatafuta Plan B, ndio kama kwenda jeshi.
 

Utapata tu ndugu, kila la kheri.
 
Pole sana. Ila geology professional is still demanding,endelea kutafuta na utapata tu. P/se usisahau kumwomba alah while unahangaika!!
 
Pole sana. Ila geology professional is still demanding,endelea kutafuta na utapata tu. P/se usisahau kumwomba alah while unahangaika!!

Ameen mkuu. Nitazingatia ushauri huu, thanks kwa kunipa moyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…