Me: Samahani ndgu zangu, mpaka kufika kuomba ushauri ni hivi, mimi ni graduate engineer katika fani ya telecom mwaka jana(2013). Shida iliyofanya nije kuomba ushauri ni hii mwez uliopita tar 16 february, nilipigiwa simu na namba ngeni ya landline ambayo ni 0...180120, hapo kweny nucta kuna namba tatu nimezificha kiusalama zaidi, ila simu ilionyesha inatokeaa Dar coz landline huwa zina region code ambazo ukiziona utajuaa hii ni ya mkoa gani, akijieleza kwa jina la Johnston akasema nimeitwa kwenye interview makao makuu ya airtel keshoo yake tar 17 february,.
Kiukweli niliwaza sana hapo nipo arusha, ile najieleza kuwa nipo arusha hakuweza kunisikia vizuri kwa sababu simu yangu ya mchina ina shida kidgo, so mara nyingi mim huwa namskia mtu aliyenipigia vizuri ila yeye aliyepiga hawezi kunisikia vizuri, yeye akaishia kusema tu kuwa ww njoo kesho saa tatu na vyeti vyako vyote bila kukosa,nhalafu akakataa simu, kinachonishangaza hapa ni kuwa kiukweli sikuwahi kuomba kazi airtel ama hata kutuma cv yeyote airtel, pili ninavyofahamu huwa airtel au hata operator yeyote iwe tigo au voda huwa hawatumii katika mawasiliano yao yote hilo nafahamu, tatu na cha ajabu baada ya kukata simu, nilibadilisha laini kwenye handset nzuri ili nimpigiee nimweleze kuwa sitoweza kufika hiyo kesho coz nipo arusha kwa sasa, ili anipe alternative ya kufanya hiyo interview akawa hapokei simu cha ajabu hiyo namba haipokelewi mpaka leo na hata nikibadilisha namba nyingine nikipiga haipokelewi japo najua landline huwa namba ya mpigaji hionekani,,,jamani naomba ushauri kama kuna mtu alishawahi kukutana na hili aniambie ,au kuna mtu ana idea na namba hii 0...180120, anielekez japo nijuee kama ni tapeli au laaah.
Kwa sababu nikijaribu kuipiga hii namba haipokelewi ili nipate kujieleza kwa kweli imenichanganya sana ,naona kama nimekosa haki yangu ya msingi kutofanya hiyo interview, naweza sema kosa ni simu yangu ya mchina,ni hayo tu wanaforum wenzangu,
Sending…