Iko hivi, tarakilishi (computer) huendeshwa na operating system kama linux, win xp au win 7, na vile vile computer ni muunganiko wa hardware mbali mbali (peripherals) ambazo zenyewe huweza kupata mawasiliano na hiyo operating system (system manager) through installed drivers. Mfano wa periherals ni kama Network cards (NIC) , sound hardwares, monitor n.k
Sasa tuje kwenye mada yetu, ni hivi kila operating system inapowekwa katika computer huwa inaendana na aina ya drivers zake, mfano ukiweka win xp operating system inabidi uwe na drivers zake , kama huna unazitafuta, ukiweka win 7 operating system the same thing applies ,yabidi utafute drivers zinazoendana nayo. Sasa mara nyingi tunapobadilisha operating system(say toka win xp kwenda win 7) ndipo problem inapoanza , mara comp haitoi sauti , mara blue tooth haifanyi kazi n.k lakini kumbe sababu ni driver zinakosekana zinazoendana na mabadiliko hayo.
Nini la kufanya: ukishaweka OS yako mpya jaribu ku-update drivers automatically, pia njia nyingine rahisi wakati unapohama toka xp kwenda win 7 tumia option ya ku upgrade, itaenda na drivers zikiwa updated. Kama method hiyo ya ku upgrade hamna kwa modeli hiyo ya comp una install kawaida na kuzitafuta driver husika mtandaoni (saa zingine unakesha usiku kucha asubuhi ndio unabahatisha kupata tena moja au 2) wakati mwingine ukigusa tu hii hapa. Drivers common/ muhimu ni: sound drivers , wireless drivers, VGA drivers na NIC drivers, hizo nyingine yategemeana na matumizi ya mtu.