Mkuu kwa hyo bajeti yako ni afadhali ununue Canter ndio utaimudu ikianza safari za kwenda gereji na kununua spea.
Ukinunua hizo za bei kubwa na ukamaliza hela likianza kukongoroka litakushinda na matokeo yake litapaki uwani na kuwa nyumba ya kuku au makumbusho.
Kwa mfano maeneo ninayoishi Mimi kule goba watu wenye canter wanatamba sana kwa kazi za kusambaza/kuuza maji yaani hazikai chini siku nzima.