You got it... Very wise and the best advice .. But for now hawezi kufanya hivi because the hasira na yeye pia kutaka kubembelezwa ...To me I see both of them , they are thinking kuwa she has right to do whatever she did or doing.. Na huyu Kaka feels the same too .. Na kutegeana pia kumo... Both wanajiweka juu.. I guess we have to watch and see it how will it ends .. Thanks..Ndiyo tatizo ya kusaidiwa kuwaza ndani ya maisha yako...So umekubali kurudiana kisa tu ulipigiwa simu na afande mwenye cheo cha Inspector...Maisha ni yako na ni wewe unaamua uishi kama upo paradiso ama kama upo jehanum...Na huwa nasema mwanaume ni kosa kubwa kununanuna kwa hiyo na wewe hadi mdomo unavuta...Ita mama bila kujali kanuna ama kavimba mweleze haya si maisha tunayoishi na nataka kwa usiku huu nieleze ni wapi nilipokukwaza na wewe umweleze kipi hupendi na unachopenda kutoka kwake...Then unganisheni mwili uwe mmoja usiku huo kesho yake na maji bafuni utawekewa karafuu..
SawasawaNasisi turudiane
Na nadhani huyo Mama alitaka suluhu ndiyo maaana akaenda kumshtaki jamaa kwenye hilo dawati ili akifika pale wamalize tofauti zao..Sasa nashindwa elewa ni nini walichokubaliana hadi kurudishana hme na wnaendelea kununiana..Kwenye ndoa bila kujali jinsia lazima mmoja ashuke na ajifanye mjinga ili maisha yaende...You got it... Very wise and the best advice .. But for now hawezi kufanya hivi because the hasira na yeye pia kutaka kubembelezwa ...To me I see both of them , they are thinking kuwa she has right to do whatever she did or doing.. Na huyu Kaka feels the same too .. Na kutegeana pia kumo... Both wanajiweka juu.. I guess we have to watch and see it how will it ends .. Thanks..
Dear ndio hivyo no one wants to be humble .. Sisi women tunapenda kubembelezwa I'm sure jamaa aki beep kidogo kwa mkewe things will be okay.. Hata mmke pia aki beep kidogo kwa mumewe things will get better. But its not good a man kununa nuna like a woman unajiaaibishe tuu bure .. Vingenevyo ammrudishe kwao tuu kwa muda hadi akiwa tayari kuongea then he can let her inn again .. Thanks..Na nadhani huyo Mama alitaka suluhu ndiyo maaana akaenda kumshtaki jamaa kwenye hilo dawati ili akifika pale wamalize tofauti zao..Sasa nashindwa elewa ni nini walichokubaliana hadi kurudishana hme na wnaendelea kununiana..Kwenye ndoa bila kujali jinsia lazima mmoja ashuke na ajifanye mjinga ili maisha yaende...
walikubaliana kutokubalianaNa nadhani huyo Mama alitaka suluhu ndiyo maaana akaenda kumshtaki jamaa kwenye hilo dawati ili akifika pale wamalize tofauti zao..Sasa nashindwa elewa ni nini walichokubaliana hadi kurudishana hme na wnaendelea kununiana..Kwenye ndoa bila kujali jinsia lazima mmoja ashuke na ajifanye mjinga ili maisha yaende...
Tuna miaka mitano kwenye ndoa,na ndoa tulifungia kwa DC SIO kanisan.kaka naomba nikuulize swali moja tuu kabla sijakushauri; mna umri gani ndani ya ndoa? na je ndoa yenu mliifungia kanisani/msikitini au kwa DC? naomba unijibu harafu ntakushauri jambo kaka
Wakati unasubiri ushindi,nakushauri ukanunue chupi ya chuma uwe unavaa wakati wa kulala,hakikisha unatunza ufunguo asije akauona.Baada ya mwezi kupita mimi na wife tukiwa tumetengana nilipigiwa simu na Afande flan mwenye cheo cha Inspector na kuniomba nifike Kesho yake saa nne hasubui, bila kuchelewa nilifika kumbe wife alikuwa amenishitaki katika dawati la jinsia. Walitusuluhisha then wakaomba nimrudishe wife nyumban, nam nilikubaliana nao na sasa kurudi. Ila sasa ni wiki sasa katu hatuongei pamoja, tuko kitanda kimoja hatuongei, hanifungulii mlango nikirud anaegeshea tu, pili chakula nakikuta chumban kwenye hotpot lkn sikigus kutokana na kushituka, najiuliza baada ya kuja akiwa mpole yeye ndo kaongeza kabisa ukali wa kukaa kimya, nam nimeamua kukaa kimya tuone mshindi ni nan.
Tuna miaka mitano kwenye ndoa,na ndoa tulifungia kwa DC SIO kanisan.
Ububu ndani ya nyumba ni sumu kali kama hulikuwa hujuwi,mashindano ya tuone nani aanze kuongea ahhh utangoja sana,vunja ukimya mpeleke kanisani kama wewe ni mkristo ama msikitini mkapate suluhu ya matatizo yenu kupitia viongozi wa dini mfurahie ndoa yenu, acha ligi ndogoBaada ya mwezi kupita mimi na wife tukiwa tumetengana nilipigiwa simu na Afande flan mwenye cheo cha Inspector na kuniomba nifike Kesho yake saa nne hasubui kitu cha police, bila kuchelewa nilifika kumbe wife alikuwa amenishitaki katika dawati la jinsia. Walitusuluhisha then wakaomba nimrudishe wife nyumban, nam nilikubaliana nao na sasa kurudi. Ila sasa ni wiki sasa katu hatuongei pamoja, tuko kitanda kimoja hatuongei, hanifungulii mlango nikirud anaegeshea tu mlango, pili chakula nakikuta chumban kwenye hotpot lkn sikigus kutokana na kukishituka, najiuliza baada ya kuja akiwa mpole yeye ndo kaongeza kabisa ukali wa kukaa kimya, nam nimeamua kukaa kimya tuone mshindi ni nan.
Ndugu soma ujumbe huu hapa chini utakusaidia
Alichosema mama kwa Kijana wake wa kiume siku moja kabla ya kufunga ndoa.
Mummy’s man!
Wewe sasa ni mwanaume. Kuanzia kesho utakuwa na mwanamke mwigine wa maisha yako. Mpishi mwingine na mtu mwingine wa kushare nae siri zako, sitakuwa mimi tena.
Mpende mwanamke wako pengine kuliko hata mimi. Kabla hujaenda jumla kuanza maisha mengine mwanangu acha nikupe maneno machache yatakayokuongoza;
Kuna siku nilikuwa sina maelewano mazuri na baba yako. Nilikuwa nikipiga kelele na kufoka hasira zilikuwa juu, nae hasira zake zilikua juu vilevile. Nikamtusi kwa kumwambia yeye ni "mpumbavu".
Alinishangaa!! Akaniuliza nathubutuje kumuita yeye mpumbavu? Hapo hapo nikamuongezea matusi mengine nikimuita mjinga, na hana busara, nilimuita majina yote mabaya.
Angalia unajua ni nini alifanya? Hakunyanyua mkono wake kunipiga. Aliondoka kimya kimya. Akabamiza mlango na kutokomea.
Mwanangu, kama baba yako angenipiga labda na kuniumiza, kunivunja either mkono au mguu, ungekaa na mimi hapa? Ungemuheshimu kama baba yako? Je ungekuwa unajivunia kuwa na baba kama yeye? Au ungenilaumu mimi kwa kumuita yale majina ya kuudhi.
Kamwe usimpige mkeo! Haijalishi amekuudhi kwa kiasi gani. Wewe kaa kimya na ondoka na mambo yatasonga. Kila atakapojaribu kuleta maudhi kumbuka haya niliyokueleza.
Kabla sijasahau, Baada ya baba yako kuondoka, nilijisikia vibaya mno. Alirudi akiwa bado na hasira. Na asubuhi siku iliyofuata nilifanya kila naloweza kumuomba msamaha.
Alinisamehe kwa moyo mweupe na siku hiyo nilimpikia chakula kizuri akipendacho, Yes najua unafahamu kuwa baba yako anapenda sana mboga za maboga zilizochanganywa na viazi mbatata.
Baada ya siku hiyo sikumuita tena majina ya kuudhi wala kumkasirisha. Heshima yangu kwake ilizidi maradufu.
Kuna kitu kikubwa cha muhimu ambacho unahitajika kukifanya kila siku, mwanangu nisikilize, mtetee mke wako.
Pale atakapokuwa under pressure simama nae kidete. Kama marafiki zako watamchukia ni jukumu lako kumfanya ajione kama ni malkia wa nguvu.
Baba zako wakubwa na wadogo hawakuwahi kunipenda, lakini baba yako siku zote alisimama upande wangu mpaka pale walipokuja kubadilika na kuniomba msamaha.
Kuna siku baba yako alikuwa mwenyeji wa mmiliki wa kampuni pamoja na wafanyakazi wenzake wawili alikokua akifanyia kazi, wote waliomba kujihifadhi hapa nyumbani kwetu.
Siku hiyo nilikuwa jikoni nikiwapikia chakula na baba yako alienda kununua vinywaji kwa ajili ya wageni. Baada ya kumaliza na kuandaa chakula mezani, kila mmoja alianza kula.
Ndipo nikakumbuka kuwa nilisahau kuweka chumvi katika chakula. Niliaibika mno mbele ya wageni. Baba yako baada ya kula tu kijiko cha kwanza alinitizama. Halafu hapohapo akawatazama wageni.
Akawaambia wageni kwamba alinipa maelekezo mwezi uliopita kwamba nisiwe naweka chumvi katika chakula kwa vile ana matatizo ya kiafya. Alizungumza hayo kwa utani mwingi na bashasha kuizima ile aibu.
Wageni walielewa na akaniomba niende nikachukue chumvi kila mmoja ajiwekee kivyake. Yeye alikula vilevile bila chumvi mpaka akamaliza. Baada ya wageni kuondoka alinihimiza tu kwa upole kuwa makini siku nyingine.
Mke wako ni kama mtoto, muda mwingine anaweza akashindwa cha kuongea au cha kufanya. Simama na ongea kwa ajili yake!
Tengeneza mazoea ya kwenda maeneo mbalimbali na mkeo, hiyo inampa ujasiri na kujiamini. Mbali na kazini, tembelea maeneo mengine na yeye.
Kama kuna mtu atakualika nyumbani kwake, au katika event yoyote ile na akakwambia usiende na mkeo kuwa makini na utumie busara.
Najua unanipenda mimi mama yako, najua huwa unanieleza matatizo na changamoto zako. Lakini kwa sasa mambo ni tofauti.
Mkeo awe wa kwanza kujua hayo kabla hujanieleza mkmi. Mwache yeye aone kabla yangu.
Kama unamatatizo nae usikimbilie kwangu. Acha siku ipite na uongee nae mwenyewe, na uombe Mungu kwa ajili ya hilo jambo.
Usishirikishe marafiki zako matatizo ya mkeo, kwao itakuwa burudani na watakucheka kinafiki kwa kushindwa kusimamia ustawi wa ndoa yako.
La mwisho, usisahau kuja kunitembelea wewe na mkeo kila mwezi. Najua utakuwa na nyumba yenye furaha, ila siku zote wewe bado ni mummy's Man.
Mungu atabariki nyumba yako na uzao wako. Usisahau kumuomba yeye na kutafuta msaada kwake.
Nimekulea katika maadili mema, Nimekusomesha, una elimu kubwa, basi ukawe mfano bora kwa kila kijana ulimwenguni, ukawatie moyo na kuwapa matumaini juu ya Ndoa.
Msingi wa taifa lolote lenye maadili huanzia katika ngazi ya familia. Hii ambayo wewe unaenda kuijenga.
Nitakupenda siku zote mwanangu, nenda na ninakutakia kila la kheri mwenyezi Mungu akubariki wewe, mkeo mtarajiwa na uzao wako.
Unamiaka mingapi mkuuBaada ya mwezi kupita mimi na wife tukiwa tumetengana nilipigiwa simu na Afande flan mwenye cheo cha Inspector na kuniomba nifike Kesho yake saa nne hasubui, bila kuchelewa nilifika kumbe wife alikuwa amenishitaki katika dawati la jinsia. Walitusuluhisha then wakaomba nimrudishe wife nyumban, nam nilikubaliana nao na sasa kurudi. Ila sasa ni wiki sasa katu hatuongei pamoja, tuko kitanda kimoja hatuongei, hanifungulii mlango nikirud anaegeshea tu, pili chakula nakikuta chumban kwenye hotpot lkn sikigus kutokana na kushituka, najiuliza baada ya kuja akiwa mpole yeye ndo kaongeza kabisa ukali wa kukaa kimya, nam nimeamua kukaa kimya tuone mshindi ni nan.