Nenda kalime Songea vijijini , maharage nako yanastawi, Alizeti inastawi maeneo mengi Tanzania tatizo ni mvua, haitaki mvua nyingi na ndiyo maana inastawi kwa wingi Dodoma na Singida ambako ni nusu jangwa.Sehemu zenye mvua nyingi alizeti inatakiwa ilimwe mwishoni mwa mvua,mfano mikoa ya Nyanda za juu kusini mvua zinaanza mwezi wa 12 zinaisha mwezi wa tano,kwahiyo inatakiwa upanda alizeti mwezi wa 3,haya ni maelezo ya jumla ukifika Kijiji husika unaweza kuwauliza wenyeji mvua zinaanza lini na zinaisha lini ,kwa sababu baadhi ya maeneo zinaweza kuanza mwezi wa 12 mwanzoni,kwingine mwezi wa 12 mwishoni na kuisha labda mwezi wa tano mwanzoni au mwezi wa tano mwishoni.