"hii inawezekanaje? tunalipa kodi ya serikali kila kitu unachokwenda kununua unalipa asilimia 18% hatuna sababu wanawake kulipia magharama ya kujifungua hospitali" amesema Moza.
Akizungumza leo Septemba 20, 2025 kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika jimboni la Kinondoni Moza amesema moja ya maeneo atakayosimamia ni kuhakikisha wajawazito wanapokwenda kujifungua hawalipi gharama yoyote.