Inawezekana huyo bibi kizee wakati anafanya makubaliano hayo na hata kipindi anachukua fedha benki hakuwa anaelewa anachokifanya kutokanan a uzee wake labda, inategemea alikuwa na umri gani, kwani inasemekana uzee ukizidi sana tabia zinabadilika mtu anarudi kwenye utoto na kufanya mambo kama mtoto! Ndio maana hata wasomi kwenye ngazi za maamuzi kama waheshimiwa Majaji kabla hata hawajafikisha umri wa kustaafu kikatiba; waki misbehave hawana budi kustaafishwa kwa mujibu wa katiba. Inawezekana kabisa huyo bibi kizee wakati anaingia huo mkataba hakuwa competent to contract, yaani not of sound mind na kupelekea mkataba huo kuwa batili. Hayo ni maoni yangu tu na sio sheria!