Kama mnajuana mkatukanane hukohuko na si ndani ya JF. Imefika wakati watu kama ninyi muwe mnakemewa kwa nguvu zote nami nachukua wasaa huu kukukemea; acha tabia za matusi. Hapa ni mahala pa hoja na si mahala pa matusi. Tukiendelea hivi itafika mahala JF itaonekana ni kijiwe cha wahuni tu wanaotukanana na kudhalilishana. Nikufahamishe ya kwamba wengi humu tunatumia majina ya bandia na tunadhani hatuwezi kujulikana ila ni kwamba unaweza kuwa treaceable wewe na mitusi yako.