Chama cha Demokrasia na Maendeleo leo kitafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika jimbo la Handeni.
Taarifa ya Mkuu wa Habari wa chama hicho Tumaini Makene inasema mkutano huo wa hadhara wa kampeni za uchaguzi Jimbo la Handeni, utakaofanyika leo jioni mjini Handeni, mkoani Tanga, utahutubiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama, JJ Mnyika kuanzia saa 8 mchana.
Mojawapo ya masuala ya atakayoyazungumzia ni uchambuzi wa uteuzi wa Baraza la Mawaziri la JPM uliotangazwa jana. Unakaribishwa sana.
mbona lowasa na sumaye hawaendi kuwasaidia wagombea wengine Wa ubunge. ie Handen wao kila cku kumpigia debe lema 2 arusha. Au hawana uhakika Wa kushinda sehem nyengine?
Pasipo kuwa na Baraza zuri lenye watendaji usitegemee kuapata hayo majibu mbadala ya matatizo yako. Utayasubiri hadi YESU atarudi wenzio wanakula kiulaniiiii wewe unapiga debe.
Lazima tukemee tupate baraza zuri lenye kuleta MABADILIKO YA KWELI TANZANIA.
Utamrudishaje Mwakyembe Wizarani!!!!!!!!!!!! Ana tuhuma ya Mabehewa Shirika la Reli na hajaongelea hata wakati wa kampeni kukanusha. Hivyo anaenda kuweka mikakati yakuiba tena.
Amepewa Wizara nyeti ili akaibe kwa kutumia mikataba feki na wawekezaji, pamoja na kutoa pesa BOT.