Hodi humu
Mimi mgeni kidogo humu, ila kwakuwa na mimi ni mkereketwa wa mahusiano acha leo nilete hoja humu kwa kujitumia kama mfano.
Binafsi nimeshaji engage kwenye mahusiano kwa muda sasa, na nimeshakuwa na wasichana wengi kidogo mpaka hapa nilipofikia (ila siyo kicheche) ni katika kukua kama wengine tu, unapita huku na kule, nilianza kuyatilia maanani mahuaiano wakati nipo chuo mwaka wa 3 na wa 4 kwasababu kabla ya hapo nilikuwa na msichana na alinipenda sana, ila kwakkuwa niliyachukulia poa tukaachana, maana nilijua yule msichana tusingeweza kufika naye mbali maana niliona future yangu ipo mbali, na yeye asingeweza kuvumilia ( imagine since 2006 mpaka leo na bado sijawa na wazo la kuona angeendelea kunisubiri kweli, lakini yeye alishaolewa since 2011, na hapa bado najiona mdogo kulingana na jinsi nilivyolelewa.
Sasa baada ya kumpata msichana mwingine 2010 nikiwa mwaka wa tatu chuo, tulianza kuishi naye kichuochuo, katika maisha yetu tulikutana na changamoto moja, huyo msichana alijiamini sana kuwa no one can drive her (to be honest, katika mahusiano ni lazima muheshiamiane, na mwanaume awe mwanaume, mwanamke awe mwanamke, na hapa ieleweke kuwa sina maana ya ku support mfumo dume) na mimi nilifanya kazi ya ziada kumelimisha kuwa lengo la mahusiano ni pamoja na kuliwazana na kufarijiana, lakini mwenzangu ilikuwa anapenda sana ugomvi, na alijitahd kujiweka jirani sana na ndugu zangu kuliko mimi, tukiwa likizo ugomvi ulikuwa ni mara kwa mara, hata mawasiliano yanapungua, lakini wakati huohuo anawasiliana sana na mama yangu kujiweka karibu, mpaka siku moja nikamueleza hivyo afanyavyo siyo vizuri maana kama hatengenezi peace na mimi, alaf anatengeneza peace na ndugu zangu akae akijua hao ndugu zangu siyo watakao muoa na wala hawana say katika maamuzi yangu ya nani nimuoe.
Lakini cha ajabu hakunielewa, na kilichokuwa kinaniudhi sana mimi, ni kuwa mara nyingi yeye ndo huwa anaanzisha ugomvi kwa kuanza kukuletea kesi za wanawake alafu ni za uongo, ukimuuliza ni mwanamke gani nina mahusiano naye, anakwambia unamjua mwenyewe, ukimuuliza nani kakuambia utaskia rafiki yako wa karibu na wala hakutajii, usiku kila siku anakesha kukagua simu yako ukiwa umelala, mnanuniana muda mrefu mpka unaamua kuhama kwa muda na wala hatakutafuta, ila nyege zikikushika inabd urudi mpoole.
Basi tukaendelea hivyo mpaka tukamaliza chuo, tulivyomaliza chuo wakati tunaendelea kusubiri majibu na graduation basi ugomvi ukawa mkubwa na mawasiliano yakapungua sana yaani tulikuwa tunakaa hata two weeks hatuwasiliani ( ifahamike kuwa huyo mdada nilikuwa nimemzidi miaka miwili na nusu, na nilimzidi mwaka mmoja kichuo, ila tulimaliza pamoja kwa sababu mimi course yangu ilikuwa ni ya miaka minne yeye mitaatu).
Wakati tupo likizo mimi nikaenda to my place of origin i.e. KLM, huko nikakutana na msichana mmoja ambaye alikuwa ndo kamaliza kidato cha sita, nilitokea kumpenda sana, maana tulianza naye urafiki wa kawaida miezi mitatu kabla sijamtongoza, kwa hicho kipindi nilimsoma kuwa ni mtu mpole na muelewa sana, so nikawa na compare na yule niliyekuwa naye nakuona big difference, hivyo nilimpiga vocal naye akatick maana alishaona dalili kitambo, hivyo tukawa tumeanza mahusiano.
Ulipotimia mwezi wa kumi na moja ikawa ndo kipindi cha graduation yetu, hivyo tukarudi chuoni, basi kwakuwa mahusiano yalikwisha dorora namimi tayari napepelea huku kwingine, hatukuweza kuwasiliana siku za mwanzoni, lakini ikabd mimi nimtafute, basi tukajikumbushia enzi, lakini cha kushangaza mara baada ya graduation tukazinguana tena, mi nimaona potelea mbali na mimi nikapotezea, ilifikia point tukaamua kuachana ile ya kawaida, ( si unajua watu wakizinguana huambiana kama vipi usinitafute, kila mtu na mambo yake na vitu kama hivyo) but kwa hiki kipindi mi nikawa serious, nimampotezea mazima maana tayari nlkkuwa na mtu mwingine.
Mwaka uliofuata mi nikaendelea na masomo ya juu, cha kushangaza siku moja miezi minne baadae ananitumia msg na kuanza kuni mind eti nime mcheat, huh!? nikapigwa na butwaa, maana nilijua mi na yeye tulishaachana. kiukweli alinisihi sana turudiane maana alipewa habari kuhusiana mimi na huyo msichana mpya, kiukweli mimk moyo wangu ulikuwa umeshahama kabisa maana nikikumbuka ule ugomvi na maneno ya ajabu aliyokuwa akiniambia wala sikutaka kurudi, pia kuna kipindi alimlalamikia sana mama yangu, mama daily akawa ananifowadia msgs alizokuwa anamtumia, niliingiwa na imani nikata nimrudie, by the time nafanya hivyo akawa amemind eti hataki kuongea na mimi tena, nikamtumia mpaka rafiki yake, lakini akazingua hata huyo rafiki yake wakawa hawaongei, hapo ndo nilipo sign out kabisa.
kuna mengi nimeyaweka kapuni.
Huyu niliyenaye sasa.
Ni miaka miwili imeshapita sasa, na tupo vizuri, niliamua kwa huyu nimuoneshe mapenzi ya dhati maana ninampenda kiukweli kutokana na kwamba si mtata, sasa huu upendo ninaomuonesha nahisi ni kama unamlevya, maana naye anakuwa na kakiburi flani hivi (ntakasolve tu lakini) ye anahisi kuwa mimi nimekamatika sana kwake sichomoki, inaweza kuwa kweli nimekamatika, ila suala la kutochomoka si kweli, mi nataka niwahakikishie wadada, ukiona mwanaume anakupenda kwa dhati USILEWE, ukilewa utamboa, na ukimboa mwanaume ni mwepesi kubadili maamuzi mpaka unaweza hisi alikuwa anapretend kukupenda (siyo wote lakini) we cha kufanya just take advantage ya kumuonesha mapenzi hata kidogo tu, maana sisi tunapenda bembelezwa sana, yaani ukifanya hivyo utapendwa mpaka uumwe, ukisikia kuhongwa dunia na vyote vilivyomo ndani, basi itakuwa ndo huko, wanaume si wavumilivu kama wanawake na hawaumii kama wanawake, kwa sababu yeye kutongoza ndo kazi yake (kumbuka hii ni human nature wala sisemi kwa maana mbaya) hivyo if u got mwanaume anayekupenda just treasure him aisee dont let him ho, maana ni wachache sana, wengi wetu hatujatulia. hii ndio maana nikasema mkipendwa pendekeni.
Huyu shemeji yenu leo kaniudhi kidogo ndo nikaona nitoe dukuduku langu huku. maana wakati mwingine hapa huwa ndo mwanzo wa kuchepuka.