Mlitongozana wenyewe, myamalize wenyewe

Claret

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
758
Reaction score
989
Katika mahusiano wawili wakutanapo hukubaliana kuwa pamoja. Wakati huu wawili hawa huwa hawaambiwi kitu na hata umbea wa mitaani huwa haupenyi kwao kwa maana wameshibana.

Mahusiano yao yanapofikia mwisho mbaya machungu, hasira, visasi na kukata tamaa hufuatana na baba yao shetwani kumaliza kila kilichopandwa.

Kumekuwa na tabia ya mwaga ugali nimwage mboga pindi wapenzi wanapoachana. Wengi hufikiria kwa kufanya hivyo wanapata faida ama faraja kumbe la! Ni kwa nini uanze kumtangaza mwenzio kwa wengine kisa mmeachana? Je hujui kufanya hivyo humkomoi mtu bali unajidhalilisha mwenyewe kwa kufeli katika uwanja wa mapenzi? Kwa nini msisitiriane ili mliyoyafanya yabaki kwenye maktaba yenu?

Huu ni ushauri tu kwa wale wanaojichoresha wakidhani sifa kuwasema wapenzi walioachana nao. Najua inauma ila ni budi kufunga sanduku la uhusiano ulioisha kwa namna ya kiungwana itakayowahifadhia heshima wote.

MLITONGOZANA SIRINI YAMALIZENI SIRINI VIVYO HIVYO.
 
Ni mpumbavu pekee anayewndekeza huo ujinga,

Halafu wahanga wa hizi mambo ni wanawake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…