Mkwe auawa akidai mahari

Mautamu hayajaisha ameyakatisha binti natakiwa kurudishwa nusu ghalama, mbona wewe ukiwa unasafiri basi likiharibikia njiani unarudishwa nauli nusu iweje jamaa mnaona sawa kunyang'anywa?

angemalizana na mke wake
amrudishe sio kupeleka pua ukweni kudai ng'ombe!

 
Mke kakimbia na hajulikani aliko ila ukweni anapafamu na ng'ombe anawaona kwa nini kudai mahari mnaona ni dhambi?

haaaa!kumbe na mke hajulikani alipo
kama kamuua je ili akadai mahari?
bora angerudi na mtt wa watu!

 
Usukumani inategemea na mahari uliyotoa, ng'ombe wawili unawaacha hata kama mtaachana baada ya siku moja, na ng'ombe wawili kwa kila mtoto aliyezaliwa, kama mtapata watoto say watano na mahari ulitoa ng'ombe kumi hapo hata mkiachana huna cha kudai.
 
haaaa!kumbe na mke hajulikani alipo
kama kamuua je ili akadai mahari?
bora angerudi na mtt wa watu!


Wewe ulikuwa unafikiri jamaa kafanya makusudi kwenda kudai mahari, alipeleka malalamiko baba mkwe akashindwa kuyatatua siku zikawa zinayoyoma jamaa anapiga sabuni tu akaamua kudai ng'ombe wake
 
Mke kakimbia na hajulikani aliko ila ukweni anapafamu na ng'ombe anawaona kwa nini kudai mahari mnaona ni dhambi?
Kwa sababu mke aliondokea kwa mmewe kiutaratibu alitakiwa amtafute kwanza huyu mwanamke na kisha amkabidhi kwa wazazi wake na wote kuridhia kwamba wameachana, hapo ndo mzee anaweza rudisha mahari kama yuko willing na kama hayuko willing anaweza akasema asubiri aliyekuwa mkewe akishaolewa mahari itakayopatikana atapewa.
 

Amemtafuta mpaka kwa wazazi wake nao wanataarifa kuwa binti katoleka kwa mme na walicho fanya kutoa taarifa na baba mkwe anampokea binti yake pasipo kumrudisha kwa mmewe unategemea nn hapo?
 
dah, kuna watu huwa hawaogopi sheria kabisa au ndio 'liwalo na liwe'? kama kusingekuwa na sheria hapa duniani kama wanyama wanavyoishi nadhani binadamu ndio angekuwa kiumbe cha kwanza kupotea kama inavyoaminika kwa
 
Wewe ulikuwa unafikiri jamaa kafanya makusudi kwenda kudai mahari, alipeleka malalamiko baba mkwe akashindwa kuyatatua siku zikawa zinayoyoma jamaa anapiga sabuni tu akaamua kudai ng'ombe wake
hata ningekua mimi mahari sirudishi!
nirudi kwny umaskini kisa!
 
baba mkwe ametoa adhabu kali
sheria lazima ichukue mkondo wake
ila mkwe nae hakua mstaarabu!

mi naona hata wewe sio mstaarabu kwa nini mnang'ang'ania jasho la mtu binti kakimbia rudisheni mahari mliyo chukua :A S shade:
 

mahari mnarudisha ya nini?

Na yeye atarudisha uroda alokula na kumpaka mwenzie mijasho kwa miaka mitatu mizima?????
 
mahari mnarudisha ya nini?

Na yeye atarudisha uroda alokula na kumpaka mwenzie mijasho kwa miaka mitatu mizima?????

Huo Uroda si walikuwa wanapeana wote, huo ndo utaratibu wenyewe, kwa sababu ingekuwa mahari hairudishwi kuna wazee wengine ni matapeli, anakula dili na mwanaye wanapata mahari kiasi fulani baada ya mwezi binti anarudi na mahari ishaliwa. Kwa hiyo mimi nadhani hawa wazee wetu wa zamani walikuwa na maana kubwa sana kufikiria na kuyatenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…