Mkunga and Mzizimkavu hapa kuna ukiritimba au vip | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkunga and Mzizimkavu hapa kuna ukiritimba au vip

Discussion in 'JF Doctor' started by kasopa, Nov 15, 2010.

 1. kasopa

  kasopa JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakunga mbona huyo jamaa analalamika katoa matatizo ya waziriwake hamjamsaidia mpaka anakuja kulalamika kule kwetu jameni mfanyieni ungwana hi FJ kaziyake kusaidia watu samahani kama nimewakwaza kwahili
  lkini mnategemewa na jamii

  Mbarikiwe wakuu
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kasopa samahani sana kwa kutokujibu hilo suala lako mimi Mwenyewe ni Mtaalam wa dawa za Mitishamba kama unavyoliona jina langu .Lakini hayo matatizo ya shemeji

  yangu mke wako ndio matatizo yaliyonipa mimi mwenyewe mwaka 2004 na nikaja kupona Mwaka 2005 na nilijaribu kutumia dawa nyingi za hospitali na nikawa nilipopona nikawa

  sijuwi ni ipi iliyoniponyesha kwa kweli sikuweza kuizingatia moyoni ni dawa ipi ambayo iliyoniponyesha lakini hivi majuzi tena maradhi yangu yalinirudia tena hayo Maradhi ya Mshipa wa nyonga unapokuwa unanibana nashindwa hata kutembea kukaa kwenye hii

  Computer yangu ya mezani Desktop Computer. Au hata kulala matatizo yaliponizi nilikwenda kwenye duka la Dawa na kuwaulizia ni dawa ipi yenge Nguvu ya kuweza kutoa

  maumivu wakanipa dawa moja inayoitwa kwa jina ni ( Diclofenac 100 mg) nikawa nakula kwa siku mara 2 kidonge kimoja Asubuhi na kidonge kimoja wakati wa kulala kwa muda wa

  siku 5 nikapona hiyo ndio dawa iliyonisaidia mimi sasa nakushauri uende kwenye duka la dawa kuiulizia hiyo dawa nafikiri shemeji yangu ( Mke wako atapona akitumia hiyo dawa)

  na mimi mwenyewe niliwahi kuulizia hayo matatizo yangu kwenye hii forums sikupata majibu nitumia dawa gani niliulizia hap waweza pia kuniona mimi hebu bonyeza hapa https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/65655-wakuu-nawaombeni-munisaidie-nina-maradhi-ya-uti-wa-mgongo.html hayo maradhi yanaitwa kwa kiingereza jina hili sciatic nerve

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  (1) Dawa ya maumivu ya Nyonga Mke wako Shemeji yangu mwambie atumie hizi dawa inshallah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu zitaweza kumsaidia.

  Atwange Gramu 6 za mbegu za harmal achanganye na maji ya Uvuguvugu glasi moja awe anakunywa kutwa mara 3 kabla ya kula kitu kila siku kwa muda wa siku 12 inshallah atapona. kila akitumia afanye hivyo.

  (2)Na ingine hii chemsha na maji Maganda ya limau kisha kuchemka awe anakunywa kutwa mara 3 glasi moja ya hayo maji kabla ya kula kitu Asubuhi,Mchana na usiku kwa muda wa siku 12 atapona inshallah.

  (3) Na ingine hii Pata Asali safi mbichi ya nyuki changanya na unga wa mbegu za Harmal gram 5 awe anakunywa kutwa mara 3 Asubuhi kijiko kimoja cha kulia wali mchana kijiko kimoja na usiku kijiko kimoja kwa muda wa siku 12 atapona inshallah. awe anafanya hivyo kila wakati anapotumia hiyo dawa.

  (4)Na hii ingine dawa ya kutibu hayo Maradhi ya nyonga Upate mafuta ya Hina uwe unamfanya masaji sehemu ile inayouma kwenye hiyo nyonga kila siku kutwa mara tatu kwa muda wa siku 12 inshallah atapona.

  (5) au hii ya mwisho upate Mafuta ya lozi (mlozi) uwe unafanya masaji kama unavyo fanya kwa kutumia mafuta ya Hina inshallah atapona.

  N.B Muhimu Dawa namba 1 Au dawa namba 3 unaweza kuchaguwa kutumia mojawapo kati ya hizo mbili sio kutumia zote 2 kwa wakati moja. Na zilizobakia waweza kutumia zote.
   
Loading...