MKONGE KUUZWA KWA ZABUNI

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555



MKOA wa Tanga na wakulima wa katani, wame kia uamuzi wa kuuza singa za mkonge kwa njia ya zabuni ikiwa ni njia ya kumaliza mvutano wa muda mrefu wa kimaslahi kati ya wakilima na wanunuzi wa zao hilo. Uamuzi huo ulikiwa juzi mjini hapa kwenye kikao cha pamoja kati ya wakulima wa zao hilo kutoka mashamba ya Hale, Ngombezi, Mwelya, Magunga na Magoma na uongozi wa Wilaya ya Korogwe na mkoa katika haa fupi ya kufungua zabuni kwa kampuni nne zilizoomba kununua zao hilo.

Katika haa hiyo iliwakutanisha viongozi wa wakulima wadogo,viongozi wa vyama vya ushirika vya wakulima wa zao la mkonge wa mashamba matano ya Korogwe na uongozi wa mkoa ukiwakilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Zena Saidi. Wengine kwenye kikao hicho ni Wawakilishi wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kisa Gwakisa, Mbunge wa Korogwe mjini, Mary Chatanda na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella jumla ya kampuni nne ziliomba zabuni ya kununua zao hilo.

Katika haa hiyo kampuni ya Dada Agriculture Investment ilishinda zabuni hiyo. Akizungumza baada ya kumtangaza mshindi wa zabuni hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe alisema uamuzi huo umekiwa baada ya mgogoro wa kimaslahi wa muda mrefu kati ya wakulima hao na kampuni ya Katani Ltd hali iliyosababisha mashamba kusimamisha uzalishaji kutokana na hali mbaya ya uchumi wa wakulima.

Gondwe alisema serikali ya mkoa iliamua kuingilia kati mgogoro huo ili kuupatia ufumbuzi ambapo baada ya mvutano wa muda mrefu ,mikataba iliyopo kati ya wakulima na kampuni ya Katani Ltd ilipitiwa upya na kukia maamuzi hayo ya mkonge kuuzwa kwa njia ya zabuni kwa kila baada ya miezi mitatu. Katika kuhakikisha maagizo ya serikali yanasimamiwa ipasavyo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kisa Gwakisa ameahidi kutoa ushirikiano katika suala la ulinzi kwa wakulima na mzabuni.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Dada Agriculture Investment, Fang Yu Song alisema watatekeleza masharti yote ya zabuni ikiwemo kununua tani zote za mkonge kwa mwezi katika mashamba yote ambapo uzalishaji ni tani 300 kwa mwezi na ameahidi kutoa ushirikiano kwa wakulima na serikali . Khalfan Juma mmoja wa wakulima kutoka shamba la mkonge la Mwelya alisema , Tumefurahi suala hili kukia mwisho kwa sababu ni mgogoro wa muda mrefu wa maslahi.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…