Abiria wote tulipigwa na butwaa, kila mtu alionekana kushangazwa na hili tukio la kutisha ,ilibidi abiria mmoja avunje ukimya "kwani hamna hata ndugu yake humu au mtu yeyote anayemjua??"
"sidhani kama alipanda na mtu, tangu naingia kwenye basi hili,mda mwingi alionekana mpweke na mtu aliyekosa amani, hata pale tuliposhuka kwa ajili ya kupata chakula cha mchana, yeye peke yake alibaki kwenye gari, hata nilipojaribu kubadilishana nae mawazo akuonyesha kutoa ushirikiano wa kutosha , ila jina lake aliniambia anaitwa lembeli" alielezea abiria mmoja aliyekaa karibu nae.
Abiria wote tulitoka nje,ndani wakabaki vijana wanne ambao walifunika ule mwili vizuri.
"Sasa tutafanyaje??, kama mnavyoona safari bado ni ndefu na giza linakaribia kuingia ,tumejaribu kupiga simu polisi kuwafahamisha kuhusu hili tukio , mtandao bado unasumbua,ebu tushauriane tunafanyaje?" Dereva wa basi aliomba ushauri kwa abiria wake.
" Giza linakaribia kuingia , na maiti ndo ipo kwenye gari,jamani tutaweza kweli kusafiri na maiti usiku? ,mimi binafsi sikubalini na hili kabisa" mama mmoja naye alichangia.
"Sasa unadhani tutafanyaje?, ivi angekuwa ndugu yako ungeongea hayo yote? ,tuwe na ubinadamu kwa hili"
" kama huu mwili hauna mwenyewe na mmesema hakuna anayemjua , kwa nini tusimzike porini halafu tukifika tuwataarifu polisi kuhusu hili tukio,maana kusafiri na maiti usiku sio mchezo, halafu ni vibaya sana kumbuka tupo kwenye chombo cha moto". abiria mwingine alichangia.
Ulitokea mgogoro kwa mda kidogo, abiria wengi walitoa lawama kwa basi kuwa Hawapo makini kwani walitakiwa kuwa na kitabu kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za abiria wao ,ikiwemo majina na sehemu wanazoishi.
badae wote walikubaliana kuwa wauzike ule mwili porini ili waendelee na safari, kwa sababu giza lilikuwa limeanza kuingia.
Vijana wapatao sita walifanya zoezi hilo na kumaliza kuuzika ule mwili,baadae wakaelekea walipo abiria wenzao kwa ajili ya kuanza safari.
Abiria wote waliingia kwenye basi kwa ajili ya kuendelea na safari, baada ya dakika chache abiria wote wakawa wameshaingia kwenye basi tayari kwa safari.
Ukimya ulitawala kwa dakika chache , ghafla abiria aliyekaa karibu na dereva alipiga kelele , abiria wote wakashtuka ,dereva alikuwa ameshakauka.....
To be continue....
Rate this story...
Kuna baadhi ya vitu nimevipunguza kidogo,pia mtanivumilia kwa mpamgilio mbovu, sina uzoefu sana na uandishi ndo najaribu...naomba maoni pleased.