Tufanyeje sasa ili kuepukana na kupanda kwa mfumuko wa bei?
Tufanyeje sasa ili kuepukana na kupanda kwa mfumuko wa bei?
Tufanyeje sasa ili kuepukana na kupanda kwa mfumuko wa bei?
nafikiri idadi ya Watanzania wanoamini kuwa "maisha bila rushwa hayawezekani" inazidi kuongezeka kwa kasi na hasa hii outputs ya shule na vyuo vyetu vya kata na yeyote anayejaribu kufundisha maadili anaonekana mwendawazimu.Wizi tu...Tukiacha wizi mbona kila kitu shwari....nchi ita nawiri we mwenyewe utashangaa !!!!
Tutampata wapi mwingine kama Mkapa? Tutampata wapi mwingine mwenye vision ya kumaliza umasikini wa Tanzania ifikapo 2025? Atatoka wapi, ndani ya CCM au nje?
Mfumuko wa bei kwa sasa haupukiki maana wakati ule tulikusanya fedha nyingi kutoka kwa wananchi zikawa za serikali ikasaidia kupunguza mfumuko. Sasa baada ya lile zoezi kufanikiwa tukanunua ndege ya rais, rada , tukajenga nyumba za viongozi kwa bei kubwa baada ya kuuza zile za awali kwa bei poa, nk
Hii ndio akili ya serikali yako ndugu mwananchi
Na zile kidogo zilizobaki Bank tukagawana kupitia EPA, Twin Towers, na Richmond
Unguja wameingia mtaani tayari lakini cha kusikitisha sio kuunganisha nguvu bali kutenganisha na wameanza na kuchoma mMakanisa. Nchi inaongeza matatizo badala ya kupunguza. Asante JKLazima wananchi waoneshe mfano kwa kuingia mtaani na kudai haki, bila kulazimishana huu mfumo uliopo utazidi kutumaliza.